Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,371
- 14,481
Ni usiku wa manane, na ndoto inanijia,
Leo hii jumanne, ndio imenitokea,
Katika kiza kinene, na wewe umenijia,
Baba tunakukumbuka,ulale pema peponi,
Ni mengi tumeongea, nilipokuwa ndotoni,
Pia ukatuusia, ya kufaa maishani,
Nami nikafurahia, pasi jua ni ndotoni,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Upendo uso kifani, baba ulituonyesha,
Ukatutoa kizani, kutufundisha maisha,
Tukapelekwa shuleni, ujinga ukakomesha,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Ulifunza uzalendo, tuijenge nchi yetu,
Ukatufunza upendo, ili iwe tunu kwetu,
Hata walo kandokando,walijifunzia kwetu,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika,
Wanao tunateseka, tunazidi kupigika,
Hayawani watusaka, himaya wameiteka,
Yote uliyokataza, wenzio wanaharibu,
Wale waliokutii, leo wamekugeuka,
Leo hawafuatilii, wote wamekengeuka,
Watoto hatutulii, twazidi Kulalamika,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Uchumi uloujenga, wenzako wauvuruga,
Wanatuona Wajinga,ndio maana watupiga,
Tena wanatusimanga,hata pasipo uoga,
Maisha yetu magumu,kila kona wamebana,
Wale maadui zetu,leo ni wetu rafiki,
Wanataka Mali zetu,waondoke nazo nduki,
Tutabaki bila kitu,kisa urafiki feki,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Wale ulowakataa,amewaleta chumbani,
Vinono wanajilia,na kuficha kibindoni,
Makapi twaambulia,sisi jama masikini,
Mali ulotuachia,zinaliwa na Wahuni,
Mara nikashitukia, ndoto imeniishia,
Nikabaki ninalia,ukiwa kutuachia,
Nani wa kutusemea,watesi kuwaondoa?,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Leo hii jumanne, ndio imenitokea,
Katika kiza kinene, na wewe umenijia,
Baba tunakukumbuka,ulale pema peponi,
Ni mengi tumeongea, nilipokuwa ndotoni,
Pia ukatuusia, ya kufaa maishani,
Nami nikafurahia, pasi jua ni ndotoni,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Upendo uso kifani, baba ulituonyesha,
Ukatutoa kizani, kutufundisha maisha,
Tukapelekwa shuleni, ujinga ukakomesha,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Ulifunza uzalendo, tuijenge nchi yetu,
Ukatufunza upendo, ili iwe tunu kwetu,
Hata walo kandokando,walijifunzia kwetu,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Tangu ulipoondoka, mambo yamebadilika,
Wanao tunateseka, tunazidi kupigika,
Hayawani watusaka, himaya wameiteka,
Yote uliyokataza, wenzio wanaharibu,
Wale waliokutii, leo wamekugeuka,
Leo hawafuatilii, wote wamekengeuka,
Watoto hatutulii, twazidi Kulalamika,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Uchumi uloujenga, wenzako wauvuruga,
Wanatuona Wajinga,ndio maana watupiga,
Tena wanatusimanga,hata pasipo uoga,
Maisha yetu magumu,kila kona wamebana,
Wale maadui zetu,leo ni wetu rafiki,
Wanataka Mali zetu,waondoke nazo nduki,
Tutabaki bila kitu,kisa urafiki feki,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,
Wale ulowakataa,amewaleta chumbani,
Vinono wanajilia,na kuficha kibindoni,
Makapi twaambulia,sisi jama masikini,
Mali ulotuachia,zinaliwa na Wahuni,
Mara nikashitukia, ndoto imeniishia,
Nikabaki ninalia,ukiwa kutuachia,
Nani wa kutusemea,watesi kuwaondoa?,
Baba tunakukumbuka, ulale pema peponi,

