WanaJF,
Hivi ni kweli anayeua kwa upanga naye atakufa kwa upanga? Kama maneno haya ni kweli basi namwomba mwenyezi Mungu yatimie kwa wale wote wanaolihujumu taifa hili kwa kuwakandamiza wanyonge na kutumia mamlaka waliyonayo kupindisha sheria,kusingizia watu na kutengeneza matukio au kesi zisizo za kweli ili wapate kufungwa magerezani!
Wanamuziki ambao ni baba na mwana,Nguza Viking na Papii Kocha mpaka sasa wanatumikia vifungo vya maisha baada ya kusingiziwa kuwalawiti watoto wanafunzi wa shule ya msingi huko Sinza! Katika kesi ambayo kwa sasa inaonekana kusahaulika taratibu kama ilivyo kawaida yetu, mwanasheria maarufu nchini Mabere Marando aliweza kuwatoa katika kifungo cha maisha watoto wawili wa Nguza Viking waliokuwa wamefungwa gerezani pamoja na baba yao!
Mpaka sasa haijulikani ni nani aliyeshinikiza na kuitengeza kesi iliyopelekea familia ya Nguza Viking kupatwa na masaibu haya ya kufungwa maisha gerezani! Ni nani mtu huyu aliyefanya yote haya? Bila shaka atakuwa ni mtu asiye na huruma na hatari sana! Kuna utata mkubwa katika kesi hii kwani mwalimu aliyesemekana kuwa ndiye aliyekuwa akiwapeleka watoto wanafunzi kulawitiwa nyumbani kwa Nguza Viking aliachiwa huru kisha baadaye alihama shule na kwenda kusikojulikana!
Bado kuna mazingira ya giza kuhusu kesi yake ilivyoendeshwa na ushahidi ulivyotolewa, kwa hivyo bado haiondoi wasiwasi wa wengi tulionao kuwa kuna mkono wa mtu......! Katika mambo ambayo Rais ajaye ataweza kujionesha kuwa ni mtetezi wa haki ni kuondokana na wingu kama hili, ikiwemo kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa
Mpaka Vasco da Gama atakapoondoka madarakani.
Kama sikosei kwa Raisi ajaye!Zacharia Hans Poppe & co walifungwa maisha na sasa wako uraiani......kwa msamaha wa Rais
Redio itakayopiga itafungiwa kwa uchochezi na kuhatarisha usalama wa nchi na kuingilia mambo ya ndani ya mkuu wa nchi na mkewe!Mpaka leo najiuliza bila kupata jibu ni kwanini ule wimbo wa SALIMA haupigwi tena redio zote nchini! Na kama hamuamini ombeni huo wimbo upigiwe redioni kama mtapigiwa!
Inatisha nini? Tena uzuri umemsaidia hata kujua mahali alipo shahidi muhimu wa kesi hii. Mimi naomba unielekeze yupo sehemu gani au nisaidie contact zake nataka kufanya mahojiano na yeye bila kuhatarisha usalama wake. Sana sana usalama wangu ndio utakuwa hatarini lakini najitoa mhanga!YULE MWALIMU YUPO MAENEO YA KIMARA/MBEZI ANAKULA KUKU.
"hii avatar yako mbona inatisha sana"
Kwa hiyo eeh Bwana, tunapokumbuka kifo na mateso ya huyo mwanao tunakutolea kikombe cha wakovu..... ili uweze kuwaokoa waonewao.. tunaomba haya kwa njia ya Kristo mwanao...............!Ee bwana, tunatangaza kifo chako, mpaka utakapo rudi.
Kwa hiyo eeh Bwana, tunapokumbuka kifo na mateso ya huyo mwanao tunakutolea kikombe cha wakovu..... ili uweze kuwaokoa waonewao.. tunaomba haya kwa njia ya Kristo mwanao...............!
Ningefurahi kupata mchango wa kisheria je hawa jamaa wanaweza kutoka kwa taratibu za kisheria (sheria inasemaje isije tukawa tunaongea kwa huruma kwa kuwa hawa jamaa tunawafahamu) au mpaka msamaha wa rais ndiyo wanaweza kutoka