Baba mzazi wa mgombea urais Amos Siyantemi

Baba mzazi wa mgombea urais Amos Siyantemi

KILYA BIYE

Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
52
Reaction score
12
Mzee Siyantemi ni Mzee maarufu sana Kanda ya ziwa,Ni mwanasiasa Mkongwe aliyeingia kwenye Siasa akitokea sekta ya Ualimu miaka ya 80,Kabla ya Ualimu mnamo mwaka 1978 aliteuliwa kuwa kiongozi wa Msafara wa Kikundi cha Wanafunzi wa Sanaa kilichosafiri hadi Denmark na kupata mafunzo huko kwa miaka miwili.

Baada ya kurudi kutoka Denmark aliingia rasmi kwenye siasa na Aligombea Ubunge Huko Magu mwaka 1985,akashinda lakini matokeo yake yalichaakachuliwa na wafuasi wa aliyekuwa Manager wa RTC MWANZA Erenest kisumo Nyanda akawa Mbunge.

Huyu ndiye aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ktk Serikali ya Rais Mwinyi,Baada ya kuona Uwezo wake ukiwa mkubwa ktka siasa,Halmashauri kuu ya CCM ilimteua kuwa Katibu wa Chama (w)huko Mwanza,akichukua nafasi ya Mzee Mashishanga aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkoa na Baadae Mkuu wa Mkoa huko Mbeya.Akiwa Mwanza licha ya kuwa katibu wilaya,Pia alikuwa Mwenyekiti bodi ya Uwanja wa CCM Kirumba.

Mzee Siyantemi alihamishiwa kwimba ambapo aliwapigania Wagombea Wa CCM KWIMBA Mzee Sakila ambaye alipata ubunge na akateuliwa kuwa NAIBU WAZIRI Wizara ya Elimu,Mwingine ni Mbunge wa Sumve Mzee Richard Ndasa ambaye mpaka sasa ni mbunge wa Sumve.

Kipindi hicho Misungwi haikuwa Wilaya hivyo Majimbo yote mawili yakuwa chini ya CCM (W)KWIMBA.Wakati Mzee Siyantemi akiwa katibu wilaya kwimba,Mwenyekiti wilaya alikuwa Marehemu Mzee Dandu,Babu yake na Mwanamuziki marehemu Cool James.Mzee Siyantemi alistaafu kazi za chama na kuanza mapumziko ya kustaafu ambayo hakudumu nayo muda mrefu.

Hii ilitokana na Uamuzi wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kumteua tena kutoka kuwa Mstaafu na kuwa katibu Ccm (w)kwa mara nyingine tena.

Akahamishiwa Sengerema maalumu kwenda kuokoa jahazi la CCM,ambayo Mbunge wake Marehem Dr shija alikuwa akipambana na Dr Masha,Huyu Dr Masha ndiye baba yake na Lawlance Masha aliyewahi kuwa waziri kijana Serikali ya Mh Rais Kikwete.

Mzee Siyantemi akiwa katibu wilaya Sengerema akisaidiana na Makada wengine waliwezesha Ubunge kubaki CCM,na mbunge akiwa Dr Masha.

Mzee Siyantemi akitumia uzoefu toka enzi za Baba wa Taifa Mwl Nyerere alimwezesha pia Mganga William Ngereja kuwa Mbunge Sengerema.Baade Mzee huyu alistaafu na sasa anaishi Sengelema.

HUYO NDIYE MZEE SIYANTEMI BABA MZAZI WA AMOS ROBERT SIYANTEMI ALIYECHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CCM

Pichani ni picha ya pamoja ya Mwl Nyerere akiwa na Viongozi wilaya ya Magu enzi hizo,Mzee Siyantemi ni Huyo aliye Nyuma katikati ya Mwalimu Nyerere na Huyo aliye vaa miwani E. mabelele

attachment.php
 

Attachments

  • 15214_631828416930328_3403554946928004171_n.jpg
    15214_631828416930328_3403554946928004171_n.jpg
    57.9 KB · Views: 2,507
we jua sijaisoma hii habari ......naona mnaanza kutuletea stori
 
Umefanya vizuri kutuonyesha baba mzazi, kesho leta picha ya mama yake na dada zake. Tutashukuru
 
Sasa baba yake anahusika nini na siasa ya sasa hivi?Hebu mnadi mgombea
 
Nilikuwa natafuta CV ya AMOS SIYANTEMI,sasa nimeipata ipo hivi,Shule ya Msingi Nyambtilwa Magu,O-level Kinango Secondary,A level Makongo High School,B.A in Political Science and Public Administration Chuo kikuu Mliman (UDSM)Pia ana post graduate ya International Relations kutoka Central for foreign Relations Kurasini Dar,Kwa sasa anasomea PHD ya uhusiano wa Kimataifa UDSM.
 
Usipojua historia japo kwa ufupi ya wagombea,siku moja mtakuja kuongozwa na IS au Banyamulenge
 
Sasa huyo baba ndio anautamani urais au vipi?
 
Nilikuwa natafuta CV ya AMOS SIYANTEMI,sasa nimeipata ipo hivi,Shule ya Msingi Nyambtilwa Magu,O-level Kinango Secondary,A level Makongo High School,B.A in Political Science and Public Administration Chuo kikuu Mliman (UDSM)Pia ana post graduate ya International Relations kutoka Central for foreign Relations Kurasini Dar,Kwa sasa anasomea PHD ya uhusiano wa Kimataifa UDSM.

Saa hizi ni nani/anafanya nini?
 
Badala ya kumnadi mgombea,wewe unamnadi baba yake.

Na wapambe wa Makongoro wakija na gia hii huyo Amos atatoka kweli?

Leta CV ya mgombea siyo ya Baba yake.


Umenivunja mbavu NDAGLA, hiki ndicho kizazi cha elimu inayopaziwa sauti kuwa imekua kwa kiasi kikubwa nchini
 
Last edited by a moderator:
Sasa unaleta stori zababa mtu na sio mtangaza nia!!!!. Itasaidia nini?
 
Back
Top Bottom