Baba mwenye wake watatu kaokoka, je ataenda nao wote kanisani?

Mar 1, 2015
43
41
Habari wana JF
Kuna baba flani hivii ni muislamu anawake watatu na wote kazaa nao.. Sasa juzi kati kaokoka.. Kanisani ataenda na wake wote watatu au itakuwaje? Ningependa kujua wakuu.
 
Hapo sasa itabidi tupitie file lake la dhambi ili tumhakiki na achague mmoja hapo na hao wiwili wabaki kama wake hewa wasubiri kuhamia Dodoma
 
ilikuwa busara ungemuuliza mwenyewe mkuu,ukisikia umbea ndio huo mkuu!
jitahidi uishi maisha yako,itapendeza sana...
Haahaaaaa aya maisha ndugu anayeuliza anahitaji kujua. Na kama ni umbea bac we ndo umekubuhu.... Bila shaka we ni mwanaume Unajua brazia... gauni ...khanga ....ndo nguo unazovaaga??? What about abortion tuambie ushatoa ngapi.??
 
hakuwa muislam huyo.no way unaweza kuujua uislam ukaokoka kuokoka ni nini kwanza? hakuna kitu kama hicho
 
anatakiwa afunge na kuomba na MUNGU atamuonesha mke atakaeishi nae
 
Habari wana JF
Kuna baba flani hivii ni muislamu anawake watatu na wote kazaa nao.. Sasa juzi kati kaokoka.. Kanisani ataenda na wake wote watatu au itakuwaje? Ningependa kujua wakuu.
Kwa waKristo mke ni mmoja. Aliwaoa kwa ndoa ya kiislam na sasa yeye amebatizwa kwa hiyo hamna ndoa hapo, kwa wote watatu. Akitokea mmoja akaamua na yeye abatizwe basi anaweza kuendelea naye kwa kufunga ndoa kanisani...ila kwa sasa lazima afanye taratibu za talaka kwa hao wake zake. Na yeye awe huru kumfuata Bwana Yesu.
 
Kwani kuwa na wake watatu ni kitu cha ajabu?.

Mbona mitume na manabii wakubwa ndani ya biblia walimiliki mke zaidi ya mmoja.

Sioni tatizo kwake.
 
Habari wana JF
Kuna baba flani hivii ni muislamu anawake watatu na wote kazaa nao.. Sasa juzi kati kaokoka.. Kanisani ataenda na wake wote watatu au itakuwaje? Ningependa kujua wakuu.
Kikatoliki angeambiwa afunge ndoa ya kanisani na mke wa kwanza na wengine akubali kulea watoto wake mama awaachie huru wapete wenza wengine. Kilokole sifahamu vizuri lakini kwasababu aliwaoa wote kabla ya kubadili dini, anaweza kufungishwa ndoa na wote watatu.
 
Hivi ni wapi kwenye bible kumeandikwa usioe mke zaidi ya mmoja? Huwa nashangaa sana hii kitu.
 
Hapo atabaki na mke wa kwanza, kama akikubali kuokoka, kama atakataa atabaki na yeyote kati yao atakae kubali kuokoka. Ataibariki ndoa yake kanisani, kama wote wataokoka, atabaki na mke mkubwa na wengine atawaacha
 
Yule wa kwanza wake atabaki Dar na yule wa pili wake atahamia nae dodoma na yule wa tatu wake atasubiri tamko la rais 2025
 
Kikatoliki angeambiwa afunge ndoa ya kanisani na mke wa kwanza na wengine akubali kulea watoto wake mama awaachie huru wapete wenza wengine. Kilokole sifahamu vizuri lakini kwasababu aliwaoa wote kabla ya kubadili dini, anaweza kufungishwa ndoa na wote watatu.
yawezekana huyo wa pili na wa tatu hawako kwenye form,kwenye dirisha dogo la usajili ngumu kupata timu tena
 
Back
Top Bottom