kzba
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 1,355
- 789
Katika hali isiyo ya kawaida baba mwenye nyumba kanisusia kodi yake yapata siku ya 15 sasa tangia kodi yangu ya awali kwisha, niliingia kwenye hii nyumba mwaka jana mwezi wa tano kwa makubaliano kuwa nitalipa kodi ya miezi 10 ingawa sikuwa tayari kwa hiyo kodi kulipa kutokana na kipato changu.
Niliomba nimpatie kodi ya miezi 6 akakataa akasema yeye anahitaji kodi ya mwaka ili anifanyie marekebisho kwenye hii nyumba, kama kuniwekea fensi na kukarabati ndani lakini kinyume na makubaliano hakutimiza wala jambo moja mpaka hii leo, akaniambia nijitahidi walau nimpe kodi ya miezi kumi ili aweze kufanya hayo marekebisho.
Kwa maelezo yake kuwa kila mpangaji anapoingia kwa hii nyumba yake sharti umpe kodi ya mwaka alafu kodi inayofuata unalipa miezi 6 ingawa ki uhalisia haifanani kabisa kwa kulipa hiyo kodi ya mwaka ila kwa kuwa nilikuwa na uhitaji wa nyumba kwa haraka kwa wakati huo nikaona siyo kesi acha nimpe tena bila mkataba coz yeye anaishi mkoani huko.
Baada ya miezi kadhaa baadae akaniambia nimmalizie ile kodi ya miezi miwili iliyobaki coz nilimpa miezi kumi kinyume na makubaliano pia coz yeye alisema tu nimpe kodi ya miezi kumi ili afanye hayo mambo tukabishana sana nikaona acha tu nimpe coz bado naendelea kuishi hapa.
Kwa kuwa yeye hakufanya yale mambo alionihaidi mi nikaufanya ule ukarabati wa ndani kwa sababu miundo mbinu mingi ilikuwa imekufa na inaonesha ilikaa muda mrefu bila mpangaji kwa makubaliano nitampatia risiti za gharama halisi ili tu deduct kwa kodi inayofuata.
Sasa kodi imeisha nataka kumtumia kodi yake ya miezi 6 anasema nimsubiri mpaka aje hii ni wiki ya pili tangia anihaidi kuja lakini hajatokea, na mambo ya pesa nafikiri wadau mnafahamu ni za kuunga unga
Je nimfanyeje huyu mtu kabla hajaleta madhara kwangu
Na kisheria ikoje kama mtu anakiuka makubaliano ingawa si kimaandishi ila nina meseji zake zote kuhusiana na haya maelezo niliotoa hapa.
Nategemea michango iliyotukuka
Asanteni.