Baba Mkwe akiwa mjini songea, aliipaki gari karibu na duka moja ili ajipatie mkate. Baada ya kujinunulia mkate wake,akaelekea liliko gari lake.
Hapo ndipo alipomkuta chizi mmoja pandikizi la mtu. Yule chizi akamwambia,'haiwezekani gari uendeshe peke yako, na mimi ni zamu yangu kuendesha!Baba mkwe akatumia ujanja, akamwambia yule chizi kwamba lile gari haliwaki mpaka isukumwe, hivyo akamshauri yule chizi aende nyuma ya gari akasukume, likiwaka atapewa aendeshe! Yule chizi akakubali kwenda nyuma kulisukuma,baba mkwe akawasha gari na kumwacha chizi asiwe na la kufanya!