Baba / Mama yako hawakupenda?

Baba / Mama yako hawakupenda?

Tanzanite klm

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
478
Reaction score
411
Habari wakuu.
Ni kosa kubwa sana kulalamika kuwa baba yako hakupendi na anakutenga kulinganisha na wototo wengine lakini amekulipia ada na kukupa mahitaji yote ya msingi lakini unakosa ule upendo kama watoto wengine.
Wazee wa zamani ni tofauti ni vijana wa sasa wakifundwa uvumilivu fulani.

Ni dhahiri shahiri yakuwa baba yako anajua kuwa wewe si mtoto wake na hilo hawezi kukuambia.

Au pengine mama ako anajua kabisa mtoto aliyemzaa alibadilishiwa bahati mbaya na hilo ni siri yake hawezi kukuambia.

PIGA GOTI SHUKURU MUNGU HAWAJAKUUWA.

WAOMBEE MIAKA MINGI MAANA Wamekulea na kukupa mahitaji ya msingi chakula, mavazi na elimu kama uwezo wanao.

Balance upendo kwao, watendee mema na usitake nawe upendwe kama mdogo wako au kaka yako.

Hawajakuambia ukweli na hawajamuambia yeyote kwa sababu wanakupenda na wanakujali.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom