Ilipoishia............
Mzee akamwambia kama unataka nikusamehe naomba urudishe michango ya kila mtu aliyechanga katika maandalizi ya send off. Dah...... Bonge la aibu!!!!!!!! ili kunusuru maisha yake ilibidi afiate maelekezo aisee. Kila shilingi ilirudi kwa mwenyewe kama ilivyochangwa na sherehe ya send off ikaishia hewani....
Endeleaa.........
Mama mtu akarudisha michango kwa kila mtu aliyechanga kwa aibu, ila hakuwa na OPTION!!!!! Pamoja na michango ya Send off kurudishwa haikuathiri vikao vya upande wa Mume mtarajiwa. Ilifika siku ya harusi binti akafunga ndoa bila uwepo wa Baba na wala baraka za baba! Baada ya harusi binti huyooo kaondoka na mumewe kurudi Dar Es Salaam. Mama na baba binti wakabaki na msala, mwisho wa siku wakasuluhishwa na wazee yakaisha.
Maisha yakasonga, JAMANI ACHENI NDOA ZINAZOSHIKILIWA NA KAMATI YA UFUNDI!!!!!!!!! Mkumbuke kuwa chanzo cha ndoa ni kamati ya ufundi, mama na binti hawakuacha kupalilia ndoa kupitia kamati ya ufundi, Kila mara mama na binti wanawasiliana. Enheee mnaendeleaje, sio sms sio calls maadamu mambo yaende sawia. Si makali ya ndoa yaakaanza kupungua, ikabidi mama mtu amtext bintiye kitu cha kufanya, ooh fanya hivi chukua hiki na hiki nedna kule na kule fanya haya yafuatayo.
Mungu si Abdallah wala Yassin, mume machale ya naniliu yakamcheza. Siku ya siku akaanza kupekua simu ya mkewe, alichokikuta hatakisahau maishani, mume alimtisha kumuUFOO SARO binti akasema yote, chanzo kikiwa ni Bi. Mkubwa. Mume akafoward zile sms zote kwenye simu yake kisha akamwambia binti tunakwenda kwenu mguu kwa mguu. Binti na mume huyooooo mpaka kwao. Akaita wazee na wazazi pia, akawaonesha ushahidi wote, ooooooohhhhhhh baba mtu kusikia hivyo kidogo apasuke, alitamani ardhi ipasuke aingie kuficha aibu. Mama ndo kabisa "presha za kupanda na kushuka moyo" kidogo afariki dunia.
Mama akakiri na kuomba msamaha yeye pamoja na binti yake, ila mume awaambia binti abaki kwanza kwao mpaka hapo atakapomuita! Mpaka leo bado ndoa hiyo haijasuluhishwa kutokana na ushirikina na mama na binti.
HIVI NANI HAPO ALIKUWA NA MAKOSA ZAIDI????? Binti kumficha baba yake kuwa kapata ujauzito, mama kumshawishi binti kwenda kwa Sangoma, baba kurudisha michango ya Send Off??????