lakini si kosa kufanya msukumo wa kuona sheria hizo za hovyo zikifanyiwa marekebisho tuwe kama nchi nyingine zilizoendelea kidemokrasia.
Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani
Kufumbia macho uozo wa sheria kandamizi ni ulofa ulopitiliza.
Hii nchi ni ya watanzania wote na siyo kikundi cha watu wachache na familia na marafiki zao ambao wanaendele kugawana vyeo mpaka siku za mwisho.
baada ya kuwashauri wapiganie tume huru ya uchaguzi wewe unawadanganya waingie mkenge tena na cctv. hivi ukiweka uzio kwako na CCTV unaweza kumzuia kibaka asikuibie kama kadhamilia?Ushauri wa bure kwa wana Ukawa na Ccm uchaguzi wa 2020 jaribuni kufunga cctv camera sehemu zote zinazojumlishwa matokeo ili wale wanaosubilia matokeo nje ya sehemu hizo wapate kuangalia live kwenye runiha hapohapo hii itasaidia kuondoa utata wa kile kinachoendelea huko ndani
Saa nyingine ujio wa aliyekuwa adui ni baraka kutoka kwa Mungu, pamoja na Mengi yaliyosemwa kuhusu Lowassa, ujio wake una impact kubwa kwenye upinzani:-
1. Ameondoa kigugumizi kilichokuwa ndani ya CCM kwamba kujiondoa ndani ya CCM ni dhambi. Baada ya yeye kuanza tuliona wengine wakifuata kama F.Sumaye.
2. Ujio wake umekisaidia Chadema kuongeza wigo wa majimbo ambayo yalikuwa kama yamemilikiwa na Wabunge fulani. Mfano Simanjiro, Monduli.
3. Kugombea kwake Urais kulisababisha taharuki ndani ya CCM na kuwafanya wasiamini kama watashinda uchaguzi lakini pia kuliongeza hamasa kwa wananchi ya kupiga kura. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia nchi hii mgombea wa upinzani akipata kura nyingi na pia mgombea wa CCM akipata kura chache chini ya asilimia 60%.
Hayo aliyoyatoa mtoa mada ni kweli lakini kwa kuwa yamewakuta wao nadhani yatatoa elimu kwa wengine waliomo madarakani kuwa sheria ni msumeno unakata kotekote. Na sisi kama binadamu hatuwezi kujua kesho yetu itatukuta tukiwa wapi.
kwani Ccm inejenga au imepora majengoKujenga makao makuu ya chama wameshindwa na ruzuku yote ile, iwe kuweka camera nchi nzima? Labda camera wapewe msaada, na wakipewa wale mchwa kina lema wataziacha bila kuuza?