Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,450
- 5,278
Imeelezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma kimekamilisha hatua muhimu ya mchakato wa ndani wa kisiasa kwa kuchuja na kupendekeza majina ya wanachama wanaowania kugombea nafasi ya ubunge katika majimbo mbalimbali ya mkoa huo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Vyanzo vya kuaminika vya Jambo TV ambavyo vimedokezwa na mmoja wa wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM mkoani Kigoma vimeeleza kuwa mchakato huu, ulioanza katika ngazi ya wilaya, ulilenga kupokea na kuchambua majina ya wagombea waliokuwa wamejitokeza katika hatua ya awali ya kuchukua kurejesha fomu, kisha kuyapitia kwa kina kabla ya kuyawasilisha ngazi ya mkoa kwa uchujaji zaidi.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika jimbo la Kigoma Mjini, wagombea waliokuwa wakichuana katika hatua ya awali walifikia tisa, lakini kupitia kikao cha wilaya, majina yaliyopendekezwa ni ya Kilumbe Shaban, Baruan Muhuza na Dkt. Ahmed Sovu. Hata hivyo, mara baada ya majina hayo kufikishwa ngazi ya mkoa, wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Kigoma walifanya uchambuzi upya na hatimaye kupendekeza majina ya Kilumbe Shaban, Baruan Muhuza na msanii maarufu anayefahamika kwa jina la Baba Levo, wakiamua kumwondoa Dkt. Sovu kwenye orodha hiyo ya mwisho.