Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ambaye anatetea kiti hicho, Kirumba Ng’enda ameongoza kwenye kura za maoni za chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika leo, akimzidi kura 88 mpinzani wake mkuu Clayton Chipando (Baba Levo).
Akitoa matokeo ya uchaguzi huo uliofanywa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu katika Kata 19 za jimbo hilo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kigoma Mjini Sadick Kibwana Kadulo amesema kuwa Ng’enda ameshinda kwa kura 2,168 akifuatiwa na Clayton Chipando aliyepata kura 2,080, Baruani Muhuza kura 264, Dkt. Ahmad Sovu kura 247, Maulid Kikondo kura 180, huku Moses Basila akipata kura 12.
Kadulo amesema kuwa kura 12 pekee ndizo ziliharibika, huku akieleza kuwa kuhusu tetesi za zilizokua zikisambaa mitandaoni za kukamatwa kwa kura feki katika baadhi ya vituo kuwa si taarifa za kweli.
Pia soma >> GE2025 - Baba Levo aangukia pua, Ng’enda aibuka mshindi Kigoma Mjini kwa kura 2,168 dhidi ya 2,080