Baba awakimbia watoto baada ya kuzaliwa kama chura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba awakimbia watoto baada ya kuzaliwa kama chura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 8, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,227
  Trophy Points: 280
  MKAZI wa Kijiji cha Ndulungu Kata ya Kaselya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Sadiki Selemani (40) ameikimbia familia yake baada ya watoto 2 kati ya 4 waliozaliwa na mke wake Mwanaharusi Juma (32) kudaiwa kuwa na umbile la chura na tabia kama za wanyama.

  Akizungumza na waandishi nyumbani kwake mama mzazi wa watoto hao Mwanaharusi Juma amesema watoto hao ambao wamezaliwa kwa nyakati tofauti wanampa taabu sana kuwatunza baada ya baba yao kuwakimbia kwenda kusikojulikana kwa muda wa miaka 3 mpaka sasa.

  Amedai kuwa watoto hao ambao wana maumbile kama ya chura wakubwa na wana matumbo makubwa, wanakula sana na hawalali.

  Wana macho makubwa, midomo mikubwa na vichwa vyao vikubwa na ndimi zao ni pana zilizochanika chanika na hazitoi sauti za kueleweka , shingo zao ni fupi sana, migongo na vifua vyao ni vipana, vidole ni vyembamba na huku rangi za ngozi zao zikiwa na madoa madoa meusi.

  Kwa mujibu wa habari toka kwa bibi wa watoto hao Asha Shabani amesesma mkwe wake Sadiki Selemani amemkimbia mke wake muda mrefu miaka 3 iliyopita na haijulikani alikokwenda kwa sababu hakuaga baada ya kuona watoto wawili kati ya 4 waliozaliwa
  walikuwa na maumbile ya ajabu tofauti na kawaida kwa kupumulia midomo badala ya pua zao kwa sababu njia za pua zao ni ndogo sana.

  Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Iddi Abubakari (Mrema) katika maelezo yake alisema watoto hao walianza kuonyesha dalili za mabadiliko miezi 6 tu baada ya kuzaliwa, hawasemi na sauti zao ni kama za chura, macho yao ni makubwa na yanazidi kuwa meupe na kuwa na mabadiliko kila siku na katika hali hiyo huenda ndio
  sababu baba yao kuwakimbia.

  “Hali yao sasa watoto hao inatisha kwa sababu wanafanana kwa mbali kama nyani lakini maumbile kuanzia kifuani hadi kichwani ni kama chura, ” alisema mwenyekiti huyo.

  Katika maelezo yake Mwenyekiti wa kitongoji hicho cha Ndulungu kati Ramadhani Senge alisema mama wa watoto hao anapata taabu sana hapati usingizi na wanakula sana usiku kucha na ametoa ripoti kijijini kusaidiwa lakini haikuwezekana.

  Amewataja watoto hao majira ya kuwa ni Alhaji Sadiki (Osama) na Abdullatifu Sadiki hata hivyo mama yao hakupata taabu katika hali ya ujauzito wao hadi kuwazaa.

  Kamanda wa Polisi mkoani humo hakuweza kupatikana kwa njia ya simu ili kuthibtisha kutokea kwa tukio hilo.

  SOURCE: DAR LEO
   
Loading...