Baba amnyonga mtoto wake kwa mikono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba amnyonga mtoto wake kwa mikono

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  WATU watatu wamefariki dunia katika matukio kadhaa tofauti, likiwamo la baba kumnyonga mwanaye kwa mikono baada ya ugomvi kati yake na mkewe.

  Wakati mauaji hayo ya kinyama yakifanyika, watu wengine watatu wamenusurika kufa akiwamo la mke kuchomwa kisu na mumewe kutokana na wivu wa mapenzi.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Frasser Kashai alisema katika Kijiji cha Kilemba wilayani Kibondo, baba alimuua mtoto wake Bahati Kabungu (15) aliyekuwa Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Kilemba kwa kumnyonga shingo hadi kufa.

  Alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku wa saa 5:00 usiku baada ya baba huyo aliyekuwa ametoka klabuni kunywa pombe kugombana na mke wake aliyekuwa amebeba mtoto mchanga mgongoni.

  Alisema kutokana na purukushani baina ya mke na mume, mtoto aliyekuwa amebebwa mgongoni alidondoka chini na ndipo marehemu Bahati alimwokota na kumbeba.

  chanzo. Baba amnyonga mtoto wake kwa mikono

  "Kuona hivyo ndipo baba yake alimwacha mkewe na kumvamia marehemu huyo na kuanza kumnyonga shingo yake hadi kufa," alisema.

  Kamanda huyo wa polisi alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya mauaji hayo na kukimbilia kusikojulikana. Alisema juhudi za polisi kumtafuta zinaendelea.

  Kamanda Kashai alisema katika tukio lingine juzi, katika Kijiji cha Basanza wilayani Kigoma, kundi la watu waliokuwa na silaha za jadi, walivamia nyumba ya Hussein Matona (48) na kuishambulia nyumba hiyo kwa mawe na kuibomoa kabisa.

  ACP Kashai anaeleza kwamba baada ya kuvamiwa, Matona alilazimika kutoka ndani ya nyumba hiyo na kutimua mbio ili kuepuka kuuawa.

  Kamanda Kashai alisema katika tukio lingine, mtu mwingine alikutwa amekufa mita kumi kutoka nyumbani kwa Matona. Mtu huyo alikuwa amekatwa taya la kushoto kwa kitu chenye ncha kali.

  Mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Windeye Thobias ambaye ni mkazi wa Kijiji hicho cha Basanza.

  Mtu mwingine mkazi wa Kijiji cha Kumubanga wilayani Kibondo alikutwa na bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba 1953 – 1995 / 7295 ikiwa na magazini moja isiyokuwa na risasi ndani.

  Matukio yote yamethibitishwa na polisi na uongozi wa hospitali. Matukio hayo yalitokea kati ya Januari 6 na 7, mwaka huu. Mtuhumiwa mmoja ashikiliwa na polisi.

  Katika tukio lingine, mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma kisu mkewe Ghati Marwa Ruhinda (45), mkazi wa Mugumu. Mama huyo alichomwa kisu sehemu ya tumboni.


  Akisimulia mkasa huo wifi wa majeruhi huyo Rebeca Ruhinda ambaye anamuuguza alisema tukio hilo lilitokea Januari 7, mwaka huu, saa 1:15 asubuhi katika eneo la darajani wakati wakielekea nyumbani.


  Pia polisi wanamsaka mkazi wa kitongoji cha Butiama Kijiji cha Masangura baada ya kudaiwa kumkata kwa panga mtoto wake sehemu ya kichwani.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapa unauza/una-nadi nini?
  Au nimepotea jukwaa?
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  omba mod aiamishe hii habari sio mahala pake
   
 4. stevoh

  stevoh JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 2,922
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wrong file! Wrong way wrong post
   
 5. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  akina mura kwa mapanga ni noma.
   
 6. Nyaubwii

  Nyaubwii JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uzi mzuri sana mkuu, ila naona kama jukwaa sio lenyewe hili.
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyegonga 'Report' ndo sababu hadi muda huu thread haijahamishwa. Mzizi Mkavu, we mkongwe hapa, kwa nini una 'misuse' jukwaa? Lemme do it!
   
Loading...