Baba akamatwa 'laivu' akifungisha ndoa mwanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba akamatwa 'laivu' akifungisha ndoa mwanafunzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoani Lindi, Mathias Chikawe akiwa amembeba mtoto Mawazo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne alipotembelea kijiji cha Mbondo wilayani Nachgingwea hivi karibuni.Kulia ni Amina mama wa mtoto huyo anayedai kuachwa na mumewe kwa sababu ya kuipenda CCM. Picha na Exuper Kachenje
  Hussein Semdoe,Kilindi
  MKAZI wa kijiji cha Kinkwembe wa miaka 67 ,katika kata ya Mkindi Wilayani hapa, (Jina linahifadhiwa), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuozesha binti yake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Jaila. Mzee huyo alikamatwa akiwa kwenye shrehe za harusi hiyo.

  Mtuhumiwa huyo ambaye alitarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Handeni jana, inadaiwa kuwa amekataa kuwasomesha Sekondari mabinti wake wawili ambao wamefaulu na kutakiwa kujiunga katika Shule hiyo iliyopo katika kata ya Jaira tarafa ya Mswaki, akitaka waolewe na wanaume.

  Wkizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti jana viongozi wa kata hiyo ya Mkindi, walisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya Ijuma iliyopita saa 11 jioni muda mfupi baada ya kumfungisha ndoa kwa mwanaume aliyotoka katika kijiji cha Kwedinguzu wilayani Handeni.

  Yusufu Machaku ambaye ni Ofisa mtendaji wa kata hiyo, alisema kuwa mzee huyo alishauriwa kwa kuonywa mara kadha na viongozi wa kijiji na kata, lakini hakutaka kuwasikiliza.

  Tulikwenda katika kituo cha polisi Mkuyu kutaka askari ili wamkamate mzazi huyo siku ya tukio, lakini tulikuta askari mmoja tu. Tukawasiliana na polisi wilaya ambao walikuja na tukaenda pale majira ya jioni na tukamkuta binti akiwa keshapambwa yupo na mume wake muda mfupi baada ya kufunga ndoa” alisema Machaku.

  “Tulikuta sherehe kubwa ikiendelea huku bwana harusi akiwa na msafara wa magari mawili na shamrashamra mbalimbali zikiendelea nyumbani kwa mzee huyo, tukawakabidhi polisi ili Sheria ichukue mkondo wake”alisema.

  Naye Mratibu wa elimu wa kata hiyo Daudi Marambo aliwataka wazazi wasipuuzie agizo la serikali la kutaka kila mwanafunzi aliyefaulu mtihani wa darasa la saba kwenda Sekondari.

  Mwanzoni mwa mwaka huu Mkuu wa wilaya hiyo Sarah Dumba ambaye sasa amehamishiwa wilayani Njombe mkoani Iringa aliwaagiza wakuu wa Sekondari kuwapokea wanafunzi wote wa kidato cha kwanza hata kama hawana ada, sare wala michango mbalimbali, ili waendelee na masomo wakati wazazi wao wakijiandaa kuwawezesha.
  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=19214
   
Loading...