Baadhi ya yaliyojiri Septemba 2017

Baadhi ya yaliyojiri Septemba 2017

calmdowndear

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
605
Reaction score
275
#1. Rais wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Tundu Lissu alivamiwa nyumbani kwake akitoka kuwakirisha Watanzania Bungeni akapigwa risasi 38 na watu wasiojulikana.


#2. Maiti 17 zakutwa katika ufukwe wa koko beach zikiwa katika viroba. Hii ni awamu ya tatu watu wanaokotwa mahali hapo vyombo vya ulinzi vinasema Matukio hayo yanasababishwa na watu wasiojulikana.


#3. Ujumbe wa Tanzania wawashangaza wamarekani kufikia katika hotel ya kifahari kupita kiasi *Double-Tree New York* wakati takwimu zinaonesha Tanzania nchi masikini sana duniani [HASHTAG]#NBC[/HASHTAG]-NewYork Sept.25


#4. Mtumbwi wenye vilipuzi uliokamatwa bandarini umetoweka katika mazingira tata....The Guardian Sept.24


#5. Dhifa ya Kitaifa kuwakamisheni wanajeshi majukumu ya umma iligeuzwa mkutano wa CCM kufanya maigizo ya kisiasa.


#6. Rais Magufuli alisema Urais ni Mateso, aliujaribu akasukumizwa kwenye Urais.


#7. Spika Ndugai aliyechangisha michango wabunge ili Lissu atibiwe baada ya yeye (Uongozi wa Bunge) na serikali kutaa asitibiwe kwa gharama za Bunge alijitokeza na Waziri wa Afya Ummy Mwaimu baada ya siku 15 kudai kuwa serikali inataka kughalimia matibabu ya Lissu wakashangaa kwanini Watanzania tunachangia gharama za Lissu kutibiwa.

#8. Rais Magufuli alisema kuwa alipoingia madarakani alikuta bei ya sukari ni Tshs.5000/- na sasa inashuka bei kwa kasi sana kwa jitihada zake.


#9. Ofisi ya umma Ikulu yageuzwa na CCM kuwa makao makuu yao kufanyia vikao vyao vya CCM bila Katibu Mkuu wao Abdulahman Kinana.


#10. Report za Kibenki zinaonesha kushuka kwa faida za Mabenki inchini kuashiria uchumi kuendelea kudorola. Faida ya CRDB robo ya pili ya mwaka 2017 ni Tshs.13.3 Billion ukilinganisha na 27.5 Billion mwaka Jana. Na NMB katika kipindi hicho imepata faida 35.3 Billion kutoka 45 Billion za mwaka jana.


Zingine kama vile mkopo wa Credit suisse etc ongezeni
 
Back
Top Bottom