Baadhi ya wanawake wako hivi

Baadhi ya wanawake wako hivi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,742
Reaction score
25,678
Baadhi ya wanawake hudhani njia pekee ya kumwonesha upendo mpenzi ni kufanya nae mapenzi tu. Ndio maana wapo baadhi ya wanawake akikupa tu penzi basi ni kama vile amejihakikishia ujira na atakudai malipo kwa njia yoyote ile.

Kumpa penzi pekee sio kiashiria cha kuwa unampenda sana. Haya ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kumfanyia mpenzi wako kuonyesha unampenda kwa dhati.

1. Mnunulie zawadi, usiwe mtu wa kusubiri tu zawadi wakati wewe hutoi. Mnunulie Tshirt nzuri, viatu, nguo za ndani au hata simu nzuri anayoipenda iwapo una pesa.

2. Mtoe out kwa ajili ya chakula na lipa bili zote, hii ni dalili tosha kuwa kumbe unamjali pia na sio lazima yeye ndio awe mtu wa kugharamia kila kitu.

3. Mtumie meseji nzuri za mapenzi, onyesha unamkumbuka mara kwa mara.

4. Mpikie chakula kizuri anachokipenda kama suprise angalau hata mara moja kwa wiki.

5. Akiwa anapitia changamoto za maisha kama ukosefu wa fedha, hakikisha unamfariji au kumsaidia kama uwezo unao.

Usiwe mtu wa kutegemea kufanyiwa mazuri ilihali wewe haumfanyii mambo ambayo yataashiria una upendo kwake.
Kama ulikua unaenda kinyume na haya badilika mdogo wangu
 
Back
Top Bottom