Adolph Jr
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 5,857
- 9,343
Kwa kweli mimi huwa sipendezwi na siasa ila hili limenivutia kuzungumzia.
Ni muda mwingine katika mizunguko yangu Leo nimeingia Jijini Mwanza.
Nilipofika nimefikia katika stend ya Buzuruga kama kawaida na ile kushuka tu katika Bus nimekutana na wakazi wakiwa katika pilika pilika za Kimaisha na pia nimeona wazazi wakiwapeleka watoto wao shuleni na kwa bahati nimeweza kusikia baadhi ya wazazi na madereva wakilalamikia maisha ya hivi sasa.
Wazazi wakilaumu kuwa hakuna elimu bure, abiria wengine,madereva na rai wanalaumu hakuna Mvua tena wakipinga uongozi huu kwa sana tu kitu ambacho ni cha kushangaza sana si kawaida kwa wakazi hawa !
Tukiwa kwenye daladala kutokea Buzuruga kwenda Buhongwa uvumilivu ulinishinda nikaamua kuwauliza baadhi ya abiria.
Kwani serikali ndo inawaletea mvua kwann msilime kilomo cha umwagiliaji hasa mkizingatia kuwa mpo pembezoni mwa Ziwa victoria..?..Majibu yao ndo yalinifanya nilete uzi huu yalikuwa hivi.
"Hivi kuna mkulima mwenye kipato cha chini anaweza kumudu kununua mashine za umwagiliaji [Genereta na Pipe] ili kuvuta maji vipi kuhusu gharama za kuchimba visima na matanki?
Elimu bure hakuna watoto wamejaa shuleni wanahitaji pesa za madawati na Mlinzi tena na pesa za ukarabati majengo chakavu na ni zaidi ya Ada. ... nimeishia kuwafariji tu kuwa tutafika kwani hakuna namna hata Kagera waliambiwa hakuna serikali ya kujengea raia hapa ulimwenguni cha maana wachape kazi tu waache lawama ....
Kama unaweza unaweza kutoa plan b kuhusu hayo maswali au kujazia majibu. ...bye. ..
Nipo njiani naelekea sengerema nikifika ntazidi kuongeza sample ya raia.