Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanatuchelewesha

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanatuchelewesha

NGOWILE

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
454
Reaction score
258
Wadau naomba mnielewe sio kwamba nina dharau bali ndivyo nionavyo. Kiukweli mimi ni mmoja kati mtu ninayependa kuona CHADEMA inashika dola na kuiongoza nchi yetu kuondokana na utawala huu dhalimu wa chama cha mapinduzi.

Katika harakati zangu nimekuwa nikijitoa kwa hali na mali pamoja na muda wangu kuijenga CHADEMA kwa kufahamu kuwa CHADEMA itajengwa na mimi na wewe na sio Dr.Slaa na Mbowe peke yao.

Katika harakati zangu hizi nimegundua kuwa viongozi wengi tulio nao katika ngazi za wilaya na mikoa hawaendani tena na kasi ya ukuaji wa CHADEMA. Sio kwamba ninawadharau la hasha ukweli ni kwamba lazima tukubali kuwa wamefanya kazi kubwa kukifikisha chama mahali kilipo sasa.

Licha ya hilo ni lazima vilevile tukubali kuwa wengi wa viongozi hawa hawana uwezo tena wa kukisogeza chama kwani hawana jipya tena.

Kipekee nimefurahi sana madaraka kushushwa kwenye kanda. Ni vyema sasa makatibu wa chama ngazi za kanda kuwashika mkono viongozi hawa ambayo wengi wao wamechoka na hawana uwezo tena wa kuipeleka CHADEMA mbali zaidi ya ilipo sasa kwani CHADEMA ni kubwa zaidi ya uwezo wao kifikra na kiuwezo.

Ni vyema sasa chama kikawa na mfumo wa kupima utendaji wa viongozi wa chama hasa makatibu ambao ni watendaji wa chama ili kukinusuru chama na kudumaa.

Ni aibu sana kukuta kata ambazo zipo maeneo yalipo ofisi za wilaya na mikoa halafu hazina uongozi.

Ninaomba viongozi waandamizi wa chama watunusuru na dhahma iliyo mbele yetu.

By mtoto wa seremala.
 
mawazo mzuri sana mkuu yamefika na yatafanyiwa kazi
cc makene
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...

we unajiendesha kwa mfumo wa buku saba siyo? ''the more nonsense you tags the more cash you will be paid''
 
Kwani chadema kunakiongozi zaisi ya zitto? Wengine wasindikizaji tu na wazandiki.
 
By Ze Marcopolo "Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai". Acha kutupotezea muda kabebe abiria barabarani kama jina lako lilivyo.
Wazo limeletwa, jadili wazo si kuleta wazo juu ya wazo. Think big Ze Marcopolo.
 
Ni kweli, wilaya nyingi hazina uongozi wa chadema uliokamilika, mfano wilaya za mbinga, namtumbo, na hata songea vijijini!
 
huu ni muda wetu wa kujipanga,wazo zuri sana mkuu.cdm itajengwa na wenye mioyo safi.HERI WENYE MOYO SAFI,MAANA HAO WATAIRITHI NCHI;zaburi
 
Back
Top Bottom