Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

Baadhi ya solutions za matatizo ya automatic gearboxes

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,383
Reaction score
9,829
Watu wengi wanaokumbana na matatizo kwenye Automatic gearbox huishia kubadili gearbox zao. Mfano wa matatizo hayo ni gearbox haitaki kushift gears, inadelay kushift gears, engine kuendelea kuzunguka katika RPM kubwa hata baada ya kukanyaga brake, gearbox kuslip, gearbox kustuck katika Neutral position, Kutopata reverse gear, vibration during gear shifting au mengine yanayofanana na hayo. Lakini je ni kweli kwamba automatic gearbox hazitengenezeki(irrepairable)?

Kwanza kabisa ni lazima ujue kwamba urefu wa maisha ya automatic gearbox unatakiwa kuwa sawa na urefu wa maisha ya gari yako kama tu unaitunza vizuri gearbox yako ingawa zinaweza kywepo service ndogondogo kama kubadili solenoids, valves, filter, Torque converter au valve body yote n.k.

Asilimia kubwa ya matatizo ya gear shifting kwenye automatic gearbox huwa yanazaliwa kutokea kwenye valve body au Torque converter(Hii sitaijadili sana japo na yenyewe inaweza kubadilishwa kama imeleta shida). Katika valve body ambayo mara nyingi hupatikana katika oil pan huwa kunakuwa na solenoids ambazo baadhi huwa zimeunganishwa na valves moja kwa moja au huwa zimewekwa katika uelekeo wa valves. Gearbox inaweza kuwa na Shifting solenoids mbili mpaka sita.

Ingawa pia zinaweza kuwepo solenoids zingine kama Lock-up solenoid, TCC solenoid na pressure solenoid. Pia sometimes unaweza kukutana na solenoids katika housing la automatic gearbox, Mfano katika baadhi ya gearboxes, TCC solenoid imefungwa upande wa nje kwenye housing.

Kazi ya hizi valves na solenoids huwa ni kuallow au kublock movement ya ATF kwa ajili ya engagement au disengagement ya gears, lock up ya Torque convertor, regulating transmission pressure n.k. Hivyo kama kuna tatizo lolote mfano solenoid kufa, kutopokea umeme unaotakiwa, poor grounding, valve kuwa dirty au valve kuisha inaweza kupelekea matatizo hasa katika shifting ya gears kwenye Automatic tranamission.

Kuharibika kwa hizi solenoids mara nyingi husababishwa na overheating katika gearbox ambayo husababishwa na vitu mbalimbali kama joto kutoka kwenye clutches, kutumia ATF ambayo haiko recommended kwa gearbox yako,kutumia ATF muda mrefu bila kuibadili hivyo kupelekea kubadilika kwa chemical properties za hiyo ATF na kuharibika kwa Torque converter sometimes huwa kunasababisha kuraise kwa joto katika gearbox.

Haya matatizo ya gear shifting yanaweza kurekebishika na kitu kizuri zaidi ni kwamba issues nyingi za Automatic gearbox unaweza kuread kwenye OBD II scanner. Lakini pia ni vizuri zaidi ukaconfirm kwa kuipima hiyo solenoid individually baada ya kupata majibu kutoka kwenye OBD II scanner. Na hii itakusaidia kujua kama ni solenoid yenyewe ndio ina shida au kama valve ndio ina shida(Hapa nazungumzia automatic transmission ambazo zinakuwa na separated valves na solenoids).

Sasa changamoto iliyopo watu wengi akipata matatizo hayo huambiwa na mafundi funga Gearbox mpya. Sawa hilo linaweza kutatua tatizo lakini lakini mtu ataingia gharama kubwa lakini pia hakutakuwa na guarantee kwenye hiyo gearbox as far as ni used kutoka kwenye gari jingine. Hizo components nilizozitaja pale juu ni rahisi zaidi kuzibadili na siyo gharama (hata kama utabadili valve body yote) ukilinganisha na kubadili the whole gearbox.

Asanteni.
 
Dah!! mtu unamadin mengi sana, sidhan kama kuna gari itakuja kwako ikaondoka haijapona aiseee, ishu ni moja tu umbaali, Mungu akujalie mambo yako yaende sawa usogee huku Dar, watu wanahangaika sana aisee.

Mimi mwenyewe niliwahi kusikia fundi akisema gearbox haitengenezeki, ikizingua inabidi ukanunue nyingine.
 
Dah....w mtu unamadin mengi sana, sidhan kama kuna gari itakuja kwako ikaondoka haijapona aiseee, ishu ni moja tu umbaali, Mungu akujalie mambo yako yaende sawa usogee huku Dar, watu wanahangaika sana aisee. M mwenyewe niliwahi kusikia fundi akisema gearbox haitengenezeki, ikizingua inabidi ukanunue nyingine.

Mkuu nashukuru

Japo siwezi kufanya kila kitu, Ila at least I can do something.

Probably mwezi wa 7 nitakuja Dar mkuu.
 
Asante sana kwa somo zuri japo sina gari lakini nimejifunza. Pindi nikinunua gari nitaitumia elimu hii
 
Gari yangu ilukuwa haibadili gear nikaipeleka kwa fundi wakafungua sample na filter na kusafisha na wakabadili Hidrolic lakini hali ikawa ile ile, wakachomoa cable ya gearbox na hapo ikawa inabadili kama kawaida wakasema nitumie hivyo hivyo kwani gear imejam.
Gear hii ni automatic haitumii umeme...unashauri nini mkuu?
 
Gari yangu ilukuwa haibadili gear nikaipeleka kwa fundi wakafungua sample na filter na kusafisha na wakabadili Hidrolic lakini hali ikawa ile ile, wakachomoa cable ya gearbox na hapo ikawa inabadili kama kawaida wakasema nitumie hivyo hivyo kwani gear imejam.
Gear hii ni automatic haitumii umeme...unashauri nini mkuu?

Kwanza sijaelewa ni cable gani ambayo wamechomoa?

Halafu hakuna gearbox ya automatic isiyotumia umeme. Ila tu zingine huwa electronically controlled.
 
Lile tatizo la gari kutoa mshindo unapota gear kutoka P kwenda D. Unasababishwa na nini??


Mkuu Bavaria Kwanza kabisa unatakiwa kufahamu kwamba yote yanayotokea ndani ya Automatic gearbox yanakuwa controlled na pressure ya fluid inayokuwa ndani ya gearbox(ATF). Maana yake ubaposhift kutoka P kwenda N kuna valves zinaopen na fluid inakuwa pressurized kuingia baadhi ya maeneo.

Mambo yafuatayo yanaweza kupelekea mshituko(jerking) wakati wa kushift kutoka kwenye N kuja kwenye D.

1. Low level ya ATF

2. High line pressure ambayo inaweza kusababishwa na clog au kuharibika kwa shift solenoid.

3. ATF imeisha muda wake. Angalia rangi ya ATF inatakiwa kuwa pink, ukikuta ni brown inaweza kuwa inafanya kazi ila inahitaji kubadilishwa, Ukikuta imekuwa nyeusi kabadilishe haraka sana maana utakaanga gearbox siku si nyingi.

Kwa sehemu kubwa yanaweza kuwa hayo.
 
Kwanza sijaelewa ni cable gani ambayo wamechomoa?

Halafu hakuna gearbox ya automatic isiyotumia umeme. Ila tu zingine huwa electronically controlled.
Ni ile inayokwenda kwenye sehemu ya 'resi' ( sehemu ya kebo ya kuvuta mafuta) mkuu, utanisamehe sizijui lugha ya kitaalam tunanukuu kwa mafundi wetu wa uswahilini tu.
 
Mkuu Bavaria Kwanza kabisa unatakiwa kufahamu kwamba yote yanayotokea ndani ya Automatic gearbox yanakuwa controlled na pressure ya fluid inayokuwa ndani ya gearbox(ATF). Maana yake ubaposhift kutoka P kwenda N kuna valves zinaopen na fluid inakuwa pressurized kuingia baadhi ya maeneo.

Mambo yafuatayo yanaweza kupelekea mshituko(jerking) wakati wa kushift kutoka kwenye N kuja kwenye D...
ATF ni mpya kabisa hata km 500 haijafika.

Labda hilo suala lingine.
 
ATF ni mpya kabisa hata km 500 haijafika.

Labda hilo suala lingine.

Kama ATF ni mpya na kila siku ukiangalia kwenye Dipstick unaona ATF haijapungua basi shida inaweza kuwa Valve kuziba au solenoid mojawapo kwenye valve body kufa.

Kama valve body iko chini kule kwenye oil pan basi kazi inaweza kuwa rahisi. Ila kama valve body iko vertical basi ni kazi ya kushusha gearbox na kufungua sehemu ya mbele ili uipate valve body.

Infact ni issue inarekebishika.
 
Mkuu nina tatizo na gari yangu ya auto wakati nikisimamisha gari na ipo silence nikatulia nayo kama dakika hivi, wakati wa kuondoka basi lazima ishtuke hivi , na tatizo hili hulipata sqnq nikiingia njia njia za mtaani ikiwa simama simama nyingi, lakini ikiwa safari ndefu tatizo linapotea, je mkuu ni jambo gano hilo au gia box inamashaka? Shukran
 
Mkuu nina tatizo na gari yangu ya auto wakati nikisimamisha gari na ipo silence nikatulia nayo kama dakika hivi, wakati wa kuondoka basi lazima ishtuke hivi , na tatizo hili hulipata sqnq nikiingia njia njia za mtaani ikiwa simama simama nyingi, lakini ikiwa safari ndefu tatizo linapotea, je mkuu ni jambo gano hilo au gia box inamashaka? Shukran

Gari kushtuka wakati wa kuondoka ni ishu ya gearbox.

Kwa hiyo tatizo linajitokeza tu ikiwa kusimama simama ni kwingi?
 
Back
Top Bottom