Baadhi ya nyumba jirani na bahari kubomolewa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,951
156,113
SERIKALI imetangaza kubomoa nyumba zote zilizojengwa ndani ya mita 60 kutoka usawa wa bahari ikiwa ni moja ya mkakati wa kuokoa maeneo oevu, fukwe ambazo zimevamiwa na kuilinda mikoko inayokatwa ovyo.

Mkakati huo unaendeshwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wizara ya Maliasili na Utalii.

Viongozi wa wizara hiyo juzi walifanya kikao kwa pamoja na kubaini kuwa fukwe nyingi nchini zimevamiwa.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Teresa Huvisa, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Mazingira Dk. Robert Ntakamulnega na Zawadi Mbwambo ambaye ni Ofisa kutoka Maliasili na Utalii.

Profesa Tibaijuka baada ya mkutano huo aliliambia gazeti hili kuwa kwa kuanzia wameanza kusoma ramani za fukwe zilizoko Kawe na Mbezi na kugundua uvamizi mkubwa umefanywa na watu kujenga makazi.

“Tunawaambia hawa waliojenga baharini wahame kabla ya tsunami kuwakumba, hatutakuwa na huruma na mtu,” alisema Profesa Tibaijuka na kusisitiza kuwa wanafanya kzi wakiwa na Baraka za Rais Kikwete “Rais ametuhakikishia kuwa hawezi kuhalalisha haramu.”

Waziri huyo alisisitiza kuwa wametoa saa 48 kwa maofisa ardhi waende kwenye maeneo hayo kupiga picha za satelaiti na watawasilisha taarifa yao kwa kikao cha makatibu wakuu kitakachofanyika kesho.

Alisema kuna watu wamemilikishwa maeneo hayo kihalali kabla ya Sheria ya Mazingira ambao watafutiwa hati miliki hizo na watabomolewa nyumba zao, lakini watalipwa fidia. Kwa wale waliopatiwa vibali kinyume cha tararibu hawatalipwa fidia.

Naye Dk. Huvisa alisema mkakati huo ni kulinda mazingira nchi nzima na fukwe zote zitakazohusika ni za nchi nzima.

“tunataka maeneo hayo yasiendelezwe kwani sheria ya mazingira inakataza, hizi fukwe kila mtu ana haki ya kwenda kuzuru sio baadhi ya watu wajihalalishie.”
 
Mmhhhh!nilikuwa nashangaa sana ninapotembelea nchi nyingine kwa mfano hongkong ukiangalia fukwe zao zinavyolindwa na zilivyowekwa katika hali ya kila mtu kutembelea nikilinganisha na fukwe zetu hasa pale mbezi beech ni kituko na uwendawazimu nyumba zimejengwa baharini watu wamemilikishwa fukwe huwezi kuingi bila idhini ya waliojenga Yale wanayoyaita hotel.kama serikali ilifanya makosa kuwamilikisha haina budi kupata hasara kuwafidia ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua waliosababisha hasara hizi kwa ukosefu wa uadilifu kwa kutoa hati ya sehemu kama hizo
 
Golden tulip iko karibu na bahari kabisa...kama kweli wana nguvu waibomoe ile..kwanza hoteli yenyewe haina hata wateja kihivyo. But ukiangalia hizo fukwe zenyewe hata wakibomoa zitabakia kua misitu tu coz najua wabongo hawatazitunza...hatuna culture hapa ya kutunza fukwe za bahari....
 
hiyo nguvu ya soda tu mbona Lukuvi aliwakabidhi orodha ya viwanja vya wazi vilivyochukuliwa na wajinga wachache na hajafanya kitu? mie huwa sipendi mtu mbabaishaji. Kama anafanya na afanye na sio polojo nyingi kwenye magazeti kisha hatuoni kitu. Mpaka dakika hii watu wanaendelea kujenga maeneo ya wazi na wao taarifa wanapelekewa mbona hawafanyi lolote?
 
Back
Top Bottom