Baadhi ya misemo na methali toka Tanzania

Baadhi ya misemo na methali toka Tanzania

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,271
Reaction score
29,934
BAADHI YA MISEMO NA
METHALI TOKA TANZANIA

1. Acha kukuna makovu ya mende (Kichaga)

Maana yake ni kwamba uache kukumbuka taabu
ya wakati uliopita.

Methali hii itafahamika vizuri
kama tukielewa kwamba hapo zamani katika
jamii zetu, mende walikuwa wanaonekana kwa
wingi katika nyumba.

Nao mende ni hodari wa
kuuma watu wakati wa usiku wakiwa wamelala.
Na pale walipouma hubaki kovu ambalo hukuna.

Lakini pia ambaye ameshaumwa na mende hao
itakuwa ni kazi bure kama atakalia kuyakuna
makovu hayo.

Methali hii hutumika kwa kuwaonya watu
wasikalie kufikiria makosa au taabu za wakati
uliopita.

2. Afadhali kuchakaza nguo kuliko akili (Kipare)

Maana yake ni kuwa hakuna kitu bora kama akili
(hekima). Mtu ambaye hana hekima ya uchi
kuliko uchi wa aina yoyote ile.

Kuwa uchi
kinguo, mtu anaweza kununua zingine. Lakini
mtu anapokuwa uchi kiakili, hakuna maarifa.

Methali hii hutumika kwa kumhurumia mtu
ambaye ameharibikiwa na akili na anafanya
majambo isivyotakiwa katika jamii.

3. Amekufa hata Mwakafwile aliacha mwana
alipokufa (Kinyakyusa)

Methali hii inatokana na mila za kibantu kukosa
mrithi ni mwisho wa ukoo na jina la ukoo. Mtoto
wa kiume huendeleza ukoo.

Ni jambo la
kusikitisha sana kutokuwa na mwana mrithi.
Maana ya methali hii ni kwamba mtu
anayehusika hana msaada wowote kutoka kwa
ndugu, jirani au mahali penginepo.

Hutumika na mtu binafsi aliyezama ndani ya
kilindi kikubwa cha matatizo, wala hana mtoto
au mtu wa karibu naye ambaye angeweza
kumsaidia.

Ni methali ya watu maskini na
wanyonge katika kuhurumiana shidani. Kama
kuunguliwa nyumba, kufiwa nk.

4. Anayetaka usawa mwisho wake uchawi
(Kikerewe)

Methali hii ina maana kwamba tukubali kuwa
binadamu budi kutofautiana.

Fulani kapata
baiskeli – lazima nami nipate, fulani kapata
nyumba – lazima nami nipate nk. Maneno kama
haya mwishowe humsukuma mtu kutumia hila
mbaya au njia zisizo za kawaida kama vile
uchawi.

Methali hii hutumika katika kuwaonya
wanopenda kujikweza.

5.Fimbo ya jirani haiui nyoka (Kiiraqw)
Ujirani ni jambo jema lakini si vizuri kutegemea
misaada yote toka kwa majirani.

Methali hii
inafundisha umuhimu wa kujitegemea na si
kutazamia kupata misaada kila uhitajipo.

Pia, ni
lazima ieleweke kwamba hakuna sheria
inayomfanya jirani atoe msaada hata kama
anaweza, yote hutegemea matakwa yake na
huwezi kubashiri ni lini atakataa kutoa msaada.

6. Fungo alikosa mkia kwa kulala (Kizigua na
kinguu)

Ipo hadithi katika hadithi za Kizigua na Kinguu
isemayo kuwa kwa sababu ya usingizi wake
Fungo alikosa au aliupoteza mkia wake.

Methali
hii inaonyesha hasara ya uzembe na kuchelewa
mara nyingi.

Hali hii inaweza kumkosesha mtu
mambo mengi mazuri au kupoteza maslahi yake
ambayo yangemfaa baadaye. Hutumika kama
onyo kwa wazembe.

7. Anayelala na mgonjwa ndiye anayejua
miugulio (Kisambaa)

Maana yake ni kwamba huwezi kujua undani wa
mtu mpaka uwe naye karibu katika uhusiano.

Hutumika kwa mtu anayejitia kujua sana mambo
ya ndani ya wengine kuliko wenyewe
wanaohusika.

8. Hohehahe hakosi siku yake (Kiha)

Maana yake ni kuwa kila mtu ana bahati yake.
Hata maskini ana siku yake ya bahati. Hutumika
kama onyo kuwa inafaa kuthamini watu kwa utu
wao na wala si kwa mali walizonazo. Mtu ni utu.

9. Kondoo wa madoadoa hawako katika jamii ya
wanadamu (Kimasai)

Wanadamu wote hawahitilafiani sana kwa
maumbile yao, na ndio maana tunaweza
kusema, binadamu wote ni sawa. Tusikiapo kitu
kisicho cha kawaida kuhusu mtu tunaweza
kutumia msemo huu kumaanisha kwamba
tumestaajabishwa na habari hizo.

Msemo huu
unatumika pia katika kukanusha habari
zisizoaminika.

10. Kucheka chongo ya mwenzio na hali yako
umefunika (Kisukuma)

Maana yake ni kuwa si vizuri kucheka makosa
ya wengine kwani huenda ukafanya makosa yale
yale na pengine una udhaifu wako ambao
wengine wanakucheka.

Hutumika katika
kuwaonya watu wanaocheka dosari au udhaifu
wa watu wengine na pengine watu wanaocheka
wenzao waliopatwa na maafa k.m. kufilisika.

11. Mbwa mwenye mnofu mdomoni hapigi
kelele (Kifipa)

Maana yake ni kama methali ya
kiswahili isemayo:- Mwenye shibe hamjui
mwenye njaa. Methali hii hutumiwa kwa
kuwasema watu ambao wana kitu na huwasahau
wale ambao hawana kitu.

Zaidi, huweza
kutumika kwa kuwaonya viongozi wanaosahau
kuwatetea wenzao baada ya kupata madaraka
na shibe.

12. Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha
(Kikwere) Mwenda usiku hapa ni sawa na mtu
ayetenda jambo ambalo kwa wakati ule wengine
hawalielewi.

Lakini mwishowe jambo hilo
lilipoonyesha mafanikio ndipo watu wakaanza
kumsifu.

Hutumika kwa mtu anayechekwa na
wenziwe juu ya jambo alitendalo iwapo wakati
ule wale wamchekeo hawaelewi usahihi wa lile
alitendalo.

13. Nguo ya mzee haikosi chawa (kimeru)

Maana yake, mzee hakosi akiba. Maana ya
methali hii itafahamika zaidi si kwa vile hali ya
uchafu ndiyo iletayo chawa, bali kwamba kwa
mzee huwa na akiba za aina aina nayo maana
yake ni ile nzuri.

Methali hii hutumika wakati
mtu anapozungumzia utajiri wa mtu mzee. Ni
kama njia ya kuwakoga wengine kwamba wakati
wote utazamie kumkuta mzee katka hali nzuri,
anayo akiba yake ambayo ameihifadhi.

14. Usidharau wakunga uzazi ungalipo (Kibena)

Wakunga ni watu wenye kuheshimiwa sana kwa
sababu ya ufundi na ujuzi wao wakati wa
kuzalisha. Kwa kuchukua umuhimu wao huo,
wanawake hushauriwa kutowadharau maadamu

wangali wanazaa, isijeikawa wakti wa kujifungua
wakakosa msaada. Matumizi ya methali hii ni
kuwaonya watu kwa ujumla wasiwe na dharau
kwa kitu ambacho kitawafaa katika maisha yao.

Zaidi kwamba, kitu kilichokusaidi wakati uliopita
usikidharau kwa vile hukitumii kwa wakati huu.

mkuki haupingwi kwenzi

asiyekuwepo hadondokewi na mti,

walimtukana bikra maria, iweje mimi?
(kihaya)

shimbonyimbe shikukundimbe chasaka
(kichaga)

nk nk, nk, nk
 
  • Thanks
Reactions: DBA
Back
Top Bottom