Baadhi ya matawi CRDB Bank inawaibia wateja wanaochukua fedha kwenye kaunta

badoo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
512
248
Hii ni Mara kadhaa nakuta CRDB kila nitakapochukua FEDHA kwenye matawi yao mawili ya KIJITONYAMA na TABATA huwa wananiibia,ukichukuwa pesa zikiwa nyingi tu wanakuibia kwa kujua kuwa hutoweza kuhisabu kiasi kikubwa ukiwa umesimama kwenye kaunta zao,kuna siku nilikuta kila kwenye milioni moja hakuna elfu 30,na pia Mara mbili kwenye tawi la KIJITONYAMA nimekuta kwenye elfu kumi kumi wamenichomekea elfu mbili mbili na kuhesabiwa Kama elfu kumi,tabia hii pia inafanyika TABATA ambapo wengi wanalalamika kwa wizi huu.
Wahusika tunaomba mlisimamie hili.
 
Kuna siku niliweka 150,000/= account jamaa kwenye deposit in slip akaweka 15,000/= nilivyoipokea kuchek nikamuuliza kwanini unafanya hivyo eti samahani then akaongeza 135,000/= usipokuwa makini unapigwa aisee. Hii ilikuwa Azikiwe.
 
Nilishapigwa sh elfu ishirini CRDB tawi la Mbezi beach.
 
Kuna siku niliweka 150,000/= account jamaa kwenye deposit in slip akaweka 15,000/= nilivyoipokea kuchek nikamuuliza kwanini unafanya hivyo eti samahani then akaongeza 135,000/= usipokuwa makini unapigwa aisee. Hii ilikuwa Azikiwe.
Sasa si amekuibia 15,000 hapo. Au aliendelea kubadilisha?
 
Pale counter kuna tangazo linasema COUNT YOUR MONEY BEFORE YOU LEAVE COUNTER. Sasa kwasabu watanzania huwa tuna haraka sana tunaishia kuibiwa. Na mimi nasema WAWAIBIE TU maana hakuna namna.
 
Kuna siku nilikuwa na hela zangu za madafu nikazihesabu mara tatu tatu kisha nikaenda kwenye moja ya maduka ya kubadilishia fedha pale jengo la IPS maeneo ya Posta, Dsm ili kupata dola za kimarekani. Ile nimemaliza tu kumpa fedha mhudumu mmoja hivi wa kiume ili nae azihesabu simu ikaita mfukoni. Kile kitendo cha kutoa simu na kumwambia aliyenipigia kwamba nitampigia baadae jamaa akawa ameshahesabu kwa mashine fungu mojawapo la milioni moja na kuniambia limepungua laki nzima. Kwa jinsi nilivyokuwa nimezihesabu fedha hizo kwa kurudiarudia nyumbani nilikuwa na hakika kwamba aliniibia wakati najibu simu.

Nilijaribu kusisitiza kuwa zilikuwa kamili nae akadai ilipungua. Nikakubali shingo upande japo mwanzo nilitaka nilianzishe lakini busara ikanituma kwamba hiyo ni sehemu nyeti na jamaa anaweza kunibadilikia na kunizulia jambo la kunitia matatani. Tangu siku hiyo nilikoma kabisa kwenda duka hilo.
 
CRDB imeanza wizi kitambo tu tangu 1996, tena tawi la Mbagala ndio tawi la wezi kuliko matawi yote duniani. Sababu iliyonifanya kuhama crdb baada ya kuona mambo 5

1. Hakuna cctv camera ktk chumba cha tela ukitofautisha na benk nyingine.
2. Mwezi mzima wananiambia bado elfu 10000, sababu nilikuwa naweka mpunga mnene.
3. Counting machine inaangalia kwao kama kioo cha dressing table
4. Wanahesabu pesa huku wanachati,sijui wanachokifanya behind.
5. Kuna dada mmoja alikuwa ananizoeazoea, mara tabasamu mara unafanya kazi gani.
 
Pale counter kuna tangazo linasema COUNT YOUR MONEY BEFORE YOU LEAVE COUNTER. Sasa kwasabu watanzania huwa tuna haraka sana tunaishia kuibiwa. Na mimi nasema WAWAIBIE TU maana hakuna namna.
Tatizo kama ni fedha nyingi kuhesabia pale counter nako kuna risk zake kwani unaweza kuwa unazihesabu na wataalamu wanaokuwa pale kwenye foleni nao wanazihesabu kwa mbali na kisha kuvamiwa njiani au huko uendako.
 
CRDB Mlimani City mule ndo balaa zaidi nyomi ile wazee wa kazi wanakaa kama wapo restaurant vile
 
Waweke mashine zigeukie watu tuone
Uongozi waweke mashine ambazo zina functionalities zote muhimu kama display ya kiasi kinachohesabiwa kwa kuonekana pande zote mbili yaani kwa cashier na yule anaehudumiwa, detection ability ya kuonyesha au kugundua aina ya major currencies mbalimbali, thamani ya noti inayohesabiwa, na pia ugunduzi wa noti feki zinazokuwa zimechomekwa na pia zenye uwezo wa kutunza kumbukumbu za kila transaction (fedha zilizohesabiwa kwa ajili ya mteja mmoja mmoja) kwa muda mrefu ili kama kuna haja ya kupata ushahidi kwa ajili ya mlalamikaji anaedai fedha kuchomolewa iwe rahisi kuangalia kwenye mashine hizo . Kuna cash counting machines zingine hazina hizo sifa zote ila baadhi tu.
 
Huo ni ukosefu wa maadili, na mtu yeyote akikosa maadili haitajalisha kama ni banker doctor teacher engineer au fundi mwashi lazima ataharibu kazi yake tuu aidha kwa udanganyifu au wizi.

Watu wengi kwenye jamii ya leo hawana maadili hata kwenye familia zao na hii ndo hupelekea hulka za ajabu ajabu kuibuka.

Mleta mada naomba nikutaarifu hujaibiwa benki tuu bali hata wale wahudumiaji wa supermarkets wanakuibia, hawa wanagonga bidhaa mara 2 kumbe unachukua moja. Wizi huu hufanyika pale mteja anapokuwa analipia bidhaa nyingi. Pia umeshaibiwa nyama kilo nyingi tuu buchani ukiagiza kilo moja robo kilo anaibakisha na kwakuwa huna cha kukuhakiki kuwa kilo imetimia basi weye unarudi nyumbani tuliii.

Sitetei wizi wa fedha ila naonesha tatizo lipo kubwa tena sana hata ukienda hotelini na bar usipokuwa makini unabambikiwa bila au unatozwa bei juu kuliko halali yake. Pia umeshawaza vituo vingapi vya mafuta vimekupimia lita hewa za mafuta na ukalipia? ????
Maadili... maadili.... maadili.... kila kitu kimeparanganyika hata mavazi yamekosewa maadili.....

Pole kwa yalokusibu. Nimejaribu kuipanua mada na kuachia memba watafakuri .

Kasie
 
Pale counter kuna tangazo linasema COUNT YOUR MONEY BEFORE YOU LEAVE COUNTER. Sasa kwasabu watanzania huwa tuna haraka sana tunaishia kuibiwa. Na mimi nasema WAWAIBIE TU maana hakuna namna.
Kwahyo utahesabu 7m mbele ya mimacho ya watu usiowajua.
 
Huo ni uzoefu wa maadili, na mtu yeyote akikosa maadili haitajalisha kama ni banker doctor teacher engineer au fundi mwashi lazima ataharibu kazi yake tuu aidha kwa udanganyifu au wizi.

Watu wengi kwenye jamii ya leo hawana maadili hata kwenye familia zao na hii ndo hupelekea hulka za ajabu ajabu kuibuka.

Mleta mada naomba nikutaarifu hujaibiwa benki tuu bali hata wale wahudumiaji wa supermarkets wanakuibia, hawa wanagonga bidhaa mara 2 kumbe unachukua moja. Wizi huu hufanyika pale mteja anapokuwa analipia bidhaa nyingi. Pia umeshaibiwa nyama kilo nyingi tuu buchani ukiagiza kilo moja robo kilo anaibakisha na kwakuwa huna cha kukuhakiki kuwa kilo imetimia basi weye unarudi nyumbani tuliii.

Sitetei wizi wa fedha ila naonesha tatizo lipo kubwa tena sana hata ukienda hotelini na bar usipokuwa makini unabambikiwa bila au unatozwa bei juu kuliko halali yake. Pia umeshawaza vituo vingapi vya mafuta vimekupimia lita hewa za mafuta na ukalipia? ????
Maadili... maadili.... maadili.... kila kitu kimeparanganyika hata mavazi yamekosewa maadili.....

Pole kwa yalokusibu. Nimejaribu kuipanua mada na kuachia memba watafakuri .

Kasie
You're absolutely right. Tatizo ni kubwa zaidi ya hilo aliloonyesha mleta mada, hatuna maadili kuanzia ngazi ya familia. Hivyo tusitegemee kuwa watu wa maadili huko maofisini.

Nchi hii ina shida nyingi, kuanzia individuals hadi kwenye taasisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom