Baadhi ya mambo yanayofukuza fedha maishani.

Augustino Fanuel Massongo

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
1,278
666
Habari, Kwa kifupi naomba kutoa elimu hii ndogo lakini muhimu sana ktk jamii ili kufikia maendeleo binafsi kwa sababu hili ndilo lengo kuu la kila mmoja wetu. Fedha ni moja kati ya nyenzo muhimu sana maishani ambapo kila kitu ili kiwe na maana kiuchumi hupimwa kwa thamani yake kifedha,(wealth is anything with money value) na ndio maana hata ktk Misahafu imeandikwa "Fedha ndio jawabu la mambo yote".
Sasa jambo moja la msingi kulitambua ni ukweli kuwa fedha zinatembea ktk Mkondo "currency" usioonekana zinatiririka kutoka ktk point ya HITAJI "demand' na kwenda ktk SURUHISHO "supply".
Katika maisha kuna watu huwa wanatafakari matatizo na kuna wengine hutafakari masuruhisho ya matatizo hayo hayo hivyo baina ya hayo makundi mawili hilo la pili hukaa ktk mwelekeo Chanya wa kuukamata mkondo au masafa ya fedha. Mtu anayetumia muda mwingi kutafakari masuruhisho anaumba "To create" na hivyo kukaa ktk possition au nafasi Chanya ktk masafa ya kifedha yaani hukaa ktk nafasi ya kitega mkondo wa fedha zinakotoka na kuja ktk nafasi aliyopo, ndio maana kuna watu wanawekeza ktk fedha 'investors" lakini pia kuna wengine ni wasaka fedha "money mongers",Kuna aina ya watu ambao Fedha huwaandama na wengine huziandama fedha huzifukuzia.
Sasa turudi ktk hoja yetu ya msingi tuone aina ya watu ambao fedha huwakimbia.

1.Watu wasiozipa Fedha heshima.
Watu wengi hawatambui kuwa moja kati ya vitu vanavyopaswa kuheshimiwa sana sana ktk maisha ni pamoja na fedha, Yaani ingekuwa vema kama Fedha zote zingeandikwa "Handle with care" Fedha zinataka special treatment kuanzia unapozitafakari, unapozipata,unavyozitunza na zaidi sana namna unavyozitumia. Katika kila jambo ambalo mtu analiwaza, kulisema, ama kulitenda husababisha mtetemo "Vibrations" ama Chanya au Hasi yaani possitive au negative vibrations sasa mtetemo chanya unavuta posibilities yaani una- attract mambo zikiwemo Fedha na kinyume chake mtetemo Hasi una expel yaani unafukuza, Sasa tuangalie mfano wa watu wasiozihesimu Fedha na hivyo kusababisha expel wakati mwingine bila hata wao wenyewe kujua,
1:1,Watu wanaokunjakunja Fedha za noti bila utaratibu; unakuta mtu
anakunjakunja noti hadi ukiipokea unachukua sekunde kadhaa
kuinyoosha ndipo uitumie
watu wa aina hii wana expel na ama kwa hakika hawatapanda ktk
madaraja ya juu"Trend" ya nguvu za kuzimiliki yaani endapo yupo ktk
daraja la kumliki maelfu atabaki hapo hapo bila kupanda ktk daraja la
kumliki malaki au mamilioni ya fedha.
1:2,Watu wanaochafua Fedha; aina ya watu kama mafundi wanaoshika
fedha huku mikono yao ikiwa michafu,wauza mkaa,wauza samaki nk,
hawa wanazitafuta fedha wakati huohuo bila kujua wanashiriki kwa kiasi
kikubwa kuzichafua ktk mzunguko, hii pia inahusisha watu wenye tabia
ya kuandika maandishi yasiyofutika ktk noti.
1:3,Watu wanaochanyata Noti wakati wa kuzihesabu na kuzipanga yaani
unakuta mtu anapanga Fedha za noti bila kujali thamani yake mfano
anapanga fedha shs 100.000= badala ya kupanga kila kibunda kwa
thamani ya noti zake yeye
anazichanganya bila utaratibu na bila kujua kuwa ana expel.
1:4, Watu wanaoacha Fedha zikazagaa hovyo nyumbani; unakuta
nyumbani Fedha hasa sarafu ziko mahali popote eti yuko bize,
tembelea nyumba za matajiri wakubwa kama utaziona fedha zake
nyumbani.
1:5,Watu wanaohesabu fedha huku wanateambea njiani; Fedha ni kama
damu ktk mkondo wake na watu wanapaswa kusikia tu kuwa
unazimiliki na sio kuziona hovyo.
2.Watu wenye MAKHUFURU "Blasphemy".
Hii nayo ni tabia nyingine inayo expel fedha, na hii tabia huwa ama ktk maneno au matendo ya mtu na mara nyingi hii wanakuwa nayo watu wanaojiita "Maskini jeuri"Hii ni hali ya kutumia Fedha kwa namna ya kufuja huku mtu anazisindikiza kwa maneno ya dharau au ya kifedhuri, au kukanyaga fedha nk wakati mtu anayafanya haya upande mwingine kuna watu wenye kuzithamini Fedha kiasi kwamba kila wanapozipata wanazifukizia ubani, udi na manemane ili ku- create mtetemo chanya wenye ku-atract mikondo ya Fedha.
3.Watu wanaonungu'nika kupita kiasi.
Aina hii ya watu huwa hawako ktk possition ya kubuni masuruhisho kumbuka kubuni ni ku-create hivyo ni kushiriki uumbaji wa mambo maishani,misahafu pia inasema "..mauti na uzima vimo ktk UWEZO wa ulimi.." tumia kinywa chako vizuri,epuka makundi ya watu walalamikaji hata kama mazingira yakoje yaani hata kama unakaa ktk jamii ambayo watu wanakufa kila siku usitumie muda mwingi kulia msibani, bali ukitafakari positively utapata kuona fursa ya biashara ya sanda au kuchonga majeneza miongoni mwa hao wanaolia ktk jamii hiyohiyo, "and you will make profitable opportunity".
Wadau nimalizie kwa kusema kanuni hizi hazifutiki na zanatuathiri ktk maisha ya kila siku bila kujali kama tunazitambua au la.
Muwe na amani.
 
Nimeanza kwa ku like baada ya kusoma tu kichwa cha habari, ntarudi baadae kumalizia.. Najua ntakutana na madini humo ndani sasa usije ukaniangusha chief
 
Umeeleza vyema ndugu na kuna hoja ambazo tukizingatia huenda zikatusaidia katika suala zima la kumiliki pesa kwa muda mrefu.
 
Ila kwa usawa huu wa JPM ni kama pesa inaheshimiwa ila haijafikia dollar. Mi nashangaa eti dollar haikunjwi na kujua isiyochakachuliwa lazima ipite kwenye mashine. Nenda kwenye madafu sasa uone wacheza kamali wanavyoziviringisha kwenye udongo na bahati mbaya kama ni udongo wa kasulu wakati wa kiangazi hutajua rangi ya mia tano wala ya buku.
 
Habari, Kwa kifupi naomba kutoa elimu hii ndogo lakini muhimu sana ktk jamii ili kufikia maendeleo binafsi kwa sababu hili ndilo lengo kuu la kila mmoja wetu. Fedha ni moja kati ya nyenzo muhimu sana maishani ambapo kila kitu ili kiwe na maana kiuchumi hupimwa kwa thamani yake kifedha,(wealth is anything with money value) na ndio maana hata ktk Misahafu imeandikwa "Fedha ndio jawabu la mambo yote".
Sasa jambo moja la msingi kulitambua ni ukweli kuwa fedha zinatembea ktk Mkondo "currency" usioonekana zinatiririka kutoka ktk point ya HITAJI "demand' na kwenda ktk SURUHISHO "supply".
Katika maisha kuna watu huwa wanatafakari matatizo na kuna wengine hutafakari masuruhisho ya matatizo hayo hayo hivyo baina ya hayo makundi mawili hilo la pili hukaa ktk mwelekeo Chanya wa kuukamata mkondo au masafa ya fedha. Mtu anayetumia muda mwingi kutafakari masuruhisho anaumba "To create" na hivyo kukaa ktk possition au nafasi Chanya ktk masafa ya kifedha yaani hukaa ktk nafasi ya kitega mkondo wa fedha zinakotoka na kuja ktk nafasi aliyopo, ndio maana kuna watu wanawekeza ktk fedha 'investors" lakini pia kuna wengine ni wasaka fedha "money mongers",Kuna aina ya watu ambao Fedha huwaandama na wengine huziandama fedha huzifukuzia.
Sasa turudi ktk hoja yetu ya msingi tuone aina ya watu ambao fedha huwakimbia.

1.Watu wasiozipa Fedha heshima.
Watu wengi hawatambui kuwa moja kati ya vitu vanavyopaswa kuheshimiwa sana sana ktk maisha ni pamoja na fedha, Yaani ingekuwa vema kama Fedha zote zingeandikwa "Handle with care" Fedha zinataka special treatment kuanzia unapozitafakari, unapozipata,unavyozitunza na zaidi sana namna unavyozitumia. Katika kila jambo ambalo mtu analiwaza, kulisema, ama kulitenda husababisha mtetemo "Vibrations" ama Chanya au Hasi yaani possitive au negative vibrations sasa mtetemo chanya unavuta posibilities yaani una- attract mambo zikiwemo Fedha na kinyume chake mtetemo Hasi una expel yaani unafukuza, Sasa tuangalie mfano wa watu wasiozihesimu Fedha na hivyo kusababisha expel wakati mwingine bila hata wao wenyewe kujua,
1:1,Watu wanaokunjakunja Fedha za noti bila utaratibu; unakuta mtu
anakunjakunja noti hadi ukiipokea unachukua sekunde kadhaa
kuinyoosha ndipo uitumie
watu wa aina hii wana expel na ama kwa hakika hawatapanda ktk
madaraja ya juu"Trend" ya nguvu za kuzimiliki yaani endapo yupo ktk
daraja la kumliki maelfu atabaki hapo hapo bila kupanda ktk daraja la
kumliki malaki au mamilioni ya fedha.
1:2,Watu wanaochafua Fedha; aina ya watu kama mafundi wanaoshika
fedha huku mikono yao ikiwa michafu,wauza mkaa,wauza samaki nk,
hawa wanazitafuta fedha wakati huohuo bila kujua wanashiriki kwa kiasi
kikubwa kuzichafua ktk mzunguko, hii pia inahusisha watu wenye tabia
ya kuandika maandishi yasiyofutika ktk noti.
1:3,Watu wanaochanyata Noti wakati wa kuzihesabu na kuzipanga yaani
unakuta mtu anapanga Fedha za noti bila kujali thamani yake mfano
anapanga fedha shs 100.000= badala ya kupanga kila kibunda kwa
thamani ya noti zake yeye
anazichanganya bila utaratibu na bila kujua kuwa ana expel.
1:4, Watu wanaoacha Fedha zikazagaa hovyo nyumbani; unakuta
nyumbani Fedha hasa sarafu ziko mahali popote eti yuko bize,
tembelea nyumba za matajiri wakubwa kama utaziona fedha zake
nyumbani.
1:5,Watu wanaohesabu fedha huku wanateambea njiani; Fedha ni kama
damu ktk mkondo wake na watu wanapaswa kusikia tu kuwa
unazimiliki na sio kuziona hovyo.
2.Watu wenye MAKHUFURU "Blasphemy".
Hii nayo ni tabia nyingine inayo expel fedha, na hii tabia huwa ama ktk maneno au matendo ya mtu na mara nyingi hii wanakuwa nayo watu wanaojiita "Maskini jeuri"Hii ni hali ya kutumia Fedha kwa namna ya kufuja huku mtu anazisindikiza kwa maneno ya dharau au ya kifedhuri, au kukanyaga fedha nk wakati mtu anayafanya haya upande mwingine kuna watu wenye kuzithamini Fedha kiasi kwamba kila wanapozipata wanazifukizia ubani, udi na manemane ili ku- create mtetemo chanya wenye ku-atract mikondo ya Fedha.
3.Watu wanaonungu'nika kupita kiasi.
Aina hii ya watu huwa hawako ktk possition ya kubuni masuruhisho kumbuka kubuni ni ku-create hivyo ni kushiriki uumbaji wa mambo maishani,misahafu pia inasema "..mauti na uzima vimo ktk UWEZO wa ulimi.." tumia kinywa chako vizuri,epuka makundi ya watu walalamikaji hata kama mazingira yakoje yaani hata kama unakaa ktk jamii ambayo watu wanakufa kila siku usitumie muda mwingi kulia msibani, bali ukitafakari positively utapata kuona fursa ya biashara ya sanda au kuchonga majeneza miongoni mwa hao wanaolia ktk jamii hiyohiyo, "and you will make profitable opportunity".
Wadau nimalizie kwa kusema kanuni hizi hazifutiki na zanatuathiri ktk maisha ya kila siku bila kujali kama tunazitambua au la.
Muwe na amani.
Maelezo mazuri.
 
Back
Top Bottom