Baadhi ya dalili za taifa liangukalo

Baadhi ya dalili za taifa liangukalo

emmanuel1976

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
301
Reaction score
80
Kutokana na nyakati tunazopitia kama taifa imenilazimu kutafakari kwa kujiuliza kuwa ni dalili gani huambatana na dola ziangukazo. Katika tafakari hiyo nimeorodhesha baadhi ya dalili hizo na pia waweza ongezea zingine kwani hizi zaweza kuwa baadhi tu.

1. Kuporomoka kwa maadili ya viongozi wa umma. (rushwa, wizi, ubadhirifu wa mali za umma).

2. Propaganda za uongo na uzushi kutiwa uhai na kuonekana kama ukweli. Hii huwafanya wananchi kudhani wanashughulikia mambo sahihi ili kupata majibu ya ukweli kumbe sivyo.

3. Kuongezeka kwa umaskini wa kipato kwa wananchi.

4. Vijana wengi kubaki mitaani pasipo ajira.

5. Viongozi wa dola wenyewe KUTOKUWA na umoja na mshikamano thabiti. Utaona wakipingana na kushambuliana kwa maneno hadharani na kwa siri. Mwana falisafa maarufu duniani Yesu Kristo aliwahi sema ufalme (taifa) ukifitinika hauwezi kusimama.

6. Kiwango cha elimu kuwa duni.

7. Viongozi wa dola hudharau viongozi wa dini na kuweka matumaini yao katika ushirikina na uchawi ama mambo yanayo fanana na hao.

8. Anasa. Hii nayo ni dalili muhimu sana kwa taifa linaloanguka. Viongozi wake hawapendi kujishughulisha kwa bidii katika kushughulikia matatizo ya jamii zao bali hutumia vibaya pesa ya umma katika anasa. Warumi walikuwa wamebobea katika kusaka anasa kwa gharama yoyote.

9. Vyombo vya dola vya ulinzi na usalama hutumika katika kuwatisha na kuwanyamazisha raia wake pale wanapodai uwajibikaji wa viongozi wao.

Ongezea dalili zingine sote tujifunze
 
Kung'oa kucha wanaharakati na kutumia nguvu nyingi kwa watu wasio na silaha,,kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kunyang'anywa silaha kma sio kuuawa kabisa
 
1.Kutungwa sheria kandamizi bila kutumuia utaratibu unaoeleweka hasa za kunyamazisha wananchi kama sheria ya vyombo vya habari na makosa ya mtandao na kuzipa adhabu kali sana.

2. Kamata kamata ya yeyote anayepingana na matakwa ya watawala na kuwashitaki kwa makosa ya uongo mfano Gwajima
 
hahahah mkuu, kuna mataifa yanayong'oa kucha raisa wake?
 
Mwandishi mmoja wa zamani kwenye kitabu cha the origins of cold war alisema kabla ya empire haijaanguka inakuwa na dalili zifuatazo na ikitokea kuanguka dola hilo halilejei tena kwenye uimara wake kama wa mwanzo

1. Kuanguka vya fedha yake kimataifa
2. Watu wake kukosa kazi
3. Kuibuka kwa vikundi au mataifa wakishutumu utawala wake unafanya makosa
4. Kupungua kwa uzalishaji mali na pato la taifa
 
1.Kutungwa sheria kandamizi bila kutumuia utaratibu unaoeleweka hasa za kunyamazisha wananchi kama sheria ya vyombo vya habari na makosa ya mtandao na kuzipa adhabu kali sana.

2. Kamata kamata ya yeyote anayepingana na matakwa ya watawala na kuwashitaki kwa makosa ya uongo mfano Gwajima

kazi kweli kweli
 
Freedom tomorrow. Hizo ni moja ya dalili halisi za dola iangukayo.
 
1.Kutungwa sheria kandamizi bila kutumuia utaratibu unaoeleweka hasa za kunyamazisha wananchi kama sheria ya vyombo vya habari na makosa ya mtandao na kuzipa adhabu kali sana.

2. Kamata kamata ya yeyote anayepingana na matakwa ya watawala na kuwashitaki kwa makosa ya uongo mfano Gwajima

Sheria za hivyo hutungwa kama njia ya kuwanyamazisha wananchi.
 
1.Kutungwa sheria kandamizi bila kutumuia utaratibu unaoeleweka hasa za kunyamazisha wananchi kama sheria ya vyombo vya habari na makosa ya mtandao na kuzipa adhabu kali sana.

2. Kamata kamata ya yeyote anayepingana na matakwa ya watawala na kuwashitaki kwa makosa ya uongo mfano Gwajima
Huyu ni ka punje ka mchanga tu katika taifa.
au na wewe umekula maharage ya wapi yuleeeeee
 
Ongezeko la mauaji ya kisiasa.

Serikali kuwa mbali na matatizo ya wananchi ama kutokujali shida za wananchi.

Kuongoza kwa vitisho, kiburi, uvunjaji wa katiba na ongezeko la umbali kati ya watawala na watawaliwa..

Oh my God.
 
Mhe. Tabby, haya mambo unayosema hapa yanaweza kuwepo tz pia?
 
Mwandishi mmoja wa zamani kwenye kitabu cha the origins of cold war alisema kabla ya empire haijaanguka inakuwa na dalili zifuatazo na ikitokea kuanguka dola hilo halilejei tena kwenye uimara wake kama wa mwanzo

1. Kuanguka vya fedha yake kimataifa
2. Watu wake kukosa kazi
3. Kuibuka kwa vikundi au mataifa wakishutumu utawala wake unafanya makosa
4. Kupungua kwa uzalishaji mali na pato la taifa

Matumizi ya vyombo vya dola kupita kiasi ( matumizi ya nguvu) kuwanyamazisha wale wanaowakosoa viongozi walioko madarakani au kutoa ushauri chanya juu ya masuala muhimu ya kitaifa ndio dalili kuu ya kushindwa kwa tawala zilizochokwa na wananchi wake. Kwa maana nyingine ni mwanzo wa udicteta, wananchi huwa hawasikilizwi na viongozi ndio hujifanya kujua suluhisho la kila tatizo.
 
Back
Top Bottom