pye Chang shen
JF-Expert Member
- Jul 11, 2016
- 11,681
- 6,382
Kweli kabisaService road/pedestrian walkways walizotolewa wamachinga sasa hivi wamejaa bodaboda, mambo ni yale yale watembea kwa miguu Msimbazi wanapita barabarani.
Hatujasema kirikuu wala canter,Kwa hiyo malori wala kirukuu zisije Kariako kupakia bidhaa?
Hizo bidhaa zina miguu kwamba zimefika hapo zenyewe na zikitaka kwenda Congo zitatembea zenyewe?
Dah wabongo!
Tulia wewe,mtoa mada hakutaja jina la mtu yyteLegacy ya Lisu kwa watanzania ni kuolewa na Amsterdam
Kweni hawajapangiwa muda maalum wa Loading na offloading?.Natabiri kero hii itashinda hata wamachinga kwa uharibifu wa barabara ambazo zote ni mpya ila hazina muda kwani milori yenyewe ni ile misemitrela.
Aah wapi!Kweni hawajapangiwa muda maalum wa Loading na offloading?.
Authorities waweke utaratibu maana Kariakoo ni Soko la Kimataifa,Wageni wengi wanafunga mzigo,wanapakia kwenye Malori makubwa na kupeleka kwenye Mataifa yao,Aah wapi!
Saa mbili asubuhi ngoma tayari zipo ndani ya kariakoo zimeshafunga baadhi ya baeabara,
Yaani bandika bandua ikitoka hili linakuja kubwa zaidi ya hilo mpaka saa sita usiku
Nasikia kila gari wahusika wanachukua 20,000 mpaka 50,000 iki wasisumbuliwe na huku wanasjmbua watumiaji wengine wa barabara yaani hili jiji watu wanakula kupita kiasi bila kujali maisha ya raia wao
Ni wazo zuriWajenge pale jangwani kama ilivyo kwa Machinga ambao watajengewa.Mizigo ishushwe pale wafanyabiashara waje wabebe wenyewe vichwani.
Wasilite utani kuna siku lori litakurupuka lije lilete headline
Kule kuwe kweupe..na nyie mnaoenda kununua mpaki Jangwani kusudi kule waonekane watu na maduka tu.
#Mawazo ya Mtanzania huru.
Hilo litawezekana tu kwa kutenga maeneo ya malori makubwa nje ya nchi na canter ndio zisombe na kupeleka huko kwenye maloriAuthorities waweke utaratibu maana Kariakoo ni Soko la Kimataifa,Wageni wengi wanafunga mzigo,wanapakia kwenye Malori makubwa na kupeleka kwenye Mataifa yao,
Pawekwe utaratibu ambao hautawaathiri Wafanyabiashara,Watembea kwa miguu,na Wasafirishaji wa Mizigo mizito Win Win kwa kila mmoja.
Asante Mkuu kwa ustaarabu wa Bongo ulivyo mbovu hata Virikuu vitakuwa kero kubwa mno.Ni wazo zuri
Ila kubeba kichwani haiwezekani,
Ni canter na kirikuu tu ziruhusiwe kuingia kariakoo
Hili ndio suluhisho na wahusika wanajua ila nadhani utekeleaji ndio shida hapa
Sijui kwa ajili ya kipato au makusanyo
Hata dar wanakera ila dar malori yamezidi katikati ya mjiMimi kero yangu ni hawa boda boda kati kati ya miji wana kera sana. Hasa arusha yani ni kupishana tu kila sehemu wanataka kupita wao