Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Bila shaka mambo mawili ambayo yalikuwa yanatumiwa na wanaojiita UKAWA ijapokuwa ulishavunjika siku nyingi yamefikia ukingoni. Uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam umefanyika ambapo ISAYA MWITA wa CHADEMA alichaguliwa kuongoza jiji hilo. Shukrani kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye aliweka mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi huo kwa vile alijua kuwa uchaguzi huo ukifanyika tu UKAWA kwisha habari yao. Hutawasoma mitandaoni, kwenye magazeti wala kuwaona runingani.
Baada ya hapo, kick nyingine ya UKAWA ilikuwa Uchaguzi wa Marudio visiwani Zanzibar. Kabla ya uchaguzi huo, kulikuwa na tambo na majigambo mengi huku wakijiaminisha kuwa Wazanzibari watasusia uchaguzi huo. Tena vitisho vikawa vinatumika kuwatisha watu wasijitokeze kupiga kura. Miongoni mwa vitisho hivyo ni pamoja na kuchoma moto nyumba za wafuasi wa CCM.
Hata hivyo, kwa baraka za Mwenyezi, uchaguzi umefanyika salama salmini na Dr Ali Mohamed Shein akachaguliwa kwa zaidi ya asilimia 91 huku CCM ikizoa viti vyote vya ubunhe baada ya CUF kufanya ujinga ambao wataujutia wa kususia uchaguzi. Kwa sasa kinachosubiriwa ni kwa Dr Shein kuunda serikali ambayo bila shaka itakuwa ni ya upande mmoja. Kikubwa zaidi ni idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura. Kati ya watu laki tano waliojiandikisha, zaidi ya laki tatu walipuuza wito wa CUF wa kususia uchaguzi na hivyo walijitokeza kupiga kura.
Baada ya kick hizo kupatiwa ufumbuzi, kwa kweli sioni mbeleni future ya upinzani. Kule Zanzibar najua CUF wameshajifuta wenyewe. Huku Bara hawa CHADEMA hawana jipya tena hasa baada ya kulikoroga kumchagua Katibu Mkuu wa Kichina ambaye hajui A, B, C za siasa za Kibongo.
Niwape pole sana wale wote ambao nafsi zao walizitoa kwa upinzani. CCM ni ile ile iliyoleta ukombozi Msumbiji, Angola, South Africa, Namibia na hata kwa majirani zetu wa kanda ya ziwa. Kama tuliweza kusimamia ukombozi wa nchi hizo, kitatushinda nini kuweka hatamu ya uongozi kwa nchi hii? Lazima Tuheshimiane