Baada ya UKAWA Mbatia atagombea wapi?

Baada ya UKAWA Mbatia atagombea wapi?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Nimejiuliza hili swali baada ya kumwona Mbatia akiwasilisha bajeti kivuli ya wizara ya fedha. Kadhalika akimshukuru kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, mh. Mbowe kwa kumteua kwenye nafasi hiyo. Mbatia ni mwanasiasa makini. UKAWA ni muungano ambao hautaishia leo. Utakwenda hadi uchaguzi mkuu ujao, na ikibidi kuchukua Dola toka ccm.

2010 Mbatia aligombea jimbo la Kawe na kushindwa na Halima Mdee. Siamini kama 2015 atatamani kugombea urais. Wala siamini kama atakwenda tena kugombea Kawe kutokana na UKAWA. Kadhalika sina hakika kama ataenda kugombea jimbo la Vunjo ambalo akipata kuwa mwakilishi wake huko nyuma. Pale Vunjo yupo Mrema (wa chadema) ambaye aligombea na Mrema wa TLP na tlp ikashinda. Siamini kama nia za Mrema wa cdm zilifutika. Bila shaka atauwinda tena uwakilishi mwakani kwani Lyatonga sina hakika kama atagombea tena, au kupewa kura za kutosha kushinds.

Mbatia anahitajika mjengoni. Atapitia jimbo gani la uchaguzi?

---------------------------------------------------------------------------------
--------------------------------------------------------------------------------
02/09/2014 | Posted by Edson Kamukara | Kitaifatangulizi | 0 comments | 2006 views

KATIKA hali ya kutapatapa kisiasa, Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), amemshtaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), akitaka ang'olewe ubunge.
Mrema, alitoa kituko hicho juzi mjini hapa, wakati Rais Kikwete alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge kujadiliana kuhusu maridhiano ya mchakato wa katiba mpya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Mrema alimwomba Rais Kikwete awaonye Mbatia na John Mrema wa CHADEMA, akidai wanamsumbua jimboni wakitaka kumng'oa katika uchaguzi ujao.
Itakumbukwa kuwa Mbatia ndiye alikuwa mbunge wa kwanza kuongoza jimbo hilo mwaka 1995 katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na John Mrema aligombea mwaka 2010 akashindwa na Mrema.
Inaelezwa kuwa, katika hali ya kuchekesha, Mrema aliacha hoja ya msingi iliyowapeleka kwa Rais na kutumbukiza malalamiko yake binafsi, akidai Mbatia ni mtu hatari kisiasa na anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuwa ameanza kampeni kabla ya wakati.
Chanzo hicho, kiliongeza kuwa Mrema alisema pamoja na kwamba Mbatia anafanya kampeni kabla ya wakati, lakini anamlaumu zaidi Rais Kikwete kwa sababu ndiye amempa jeuri baada ya kumteua kuwa mbunge.
"Alipokuwa akisema hayo, Rais alicheka kweli kweli maana ilikuwa kama Sinema, kwa sababu alikuwa akizungumza kwa msisitizo akionyesha kukerwa na Mbatia zaidi," kilisema chanzo hicho.
Kwamba, Rais Kikwete katika kumpooza, alimtaka Mrema asiwe na wasiwasi kwa sababu wananchi wa Vunjo wanamjua mbunge wao ni nani kati yake na Mbatia.
"Rais alimuuliza kuwa kama akimwondoa Mbatia halafu akaja mwingine akamteua tena itakuwaje, lakini Mrema alishinikiza akitaka amwondoe tu na kusisitiza kwamba asipomtoa atakuwa hamtendei haki," alisema mtoa taarifa.
Alikizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mbatia alikiri kushutumiwa na Mrema mbele ya Rais na kusema kuwa hiyo ni mara ya pili kufanya hivyo hadharani.
"Ni kweli alilalamika kwa Kikwete, na hii si mara yake ya kwanza kwani hata Agosti 2 mwaka huu, alinilalamikia katika kikao cha TCD.
"Namheshimu sana Mrema, ila namuomba aendelee kuwatumikia wananchi wa Vunjo lakini kwa kuwa anazidi kunifuatafuata, Septemba 6 mwaka huu, nitahutubia mkutano wa hadhara huko Vunjo kueleza msimamo wangu," alisema Mbatia.
Naye Mrema, alisema alilazimika kumfikishia kilio chake Rais Kikwete kwa sababu ndiye alimteua Mbatia.
"Mbati ni mtu hatari sana, yaani anakwenda jimboni na kuwaambia wananchi mimi ni mzee na kibaya zaidi anasema tumekubaliana nimwachie jimbo.
"Nilimsema kwa Rais kwa sababu ananifanyia rafu kule jimboni, ni hatari sana," alisema Mrema.
Hivi karibuni, Mbatia alitangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo huku John Mrema wa CHADEMA naye akiamini kwamba uchaguzi ujao atashinda kiti hicho.
 
2015 UKAWA watachinjana wenyewe kwa wenyewe, majimbo ya CCM yatabaki kuwa ya CCM
 
The best alternative ni jimbo la VUNJO ambako aliwahi kuwa mbunge. Alibugi kwenda Kawe, Huyo Mrema wa CDM itabidi awe sacrificed, na hizo ndiyo cost za USHIRIKIANO WA VYAMA. They can learn from Kenya huwa wanafanya vipi.
 
Vunjo panamfaa sana tunamkubali aje tu hata mm nitampigia debe bure
 
Nimejiuliza hili swali baada ya kumwona Mbatia akiwasilisha bajeti kivuli ya wizara ya fedha. Kadhalika akimshukuru kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, mh. Mbowe kwa kumteua kwenye nafasi hiyo. Mbatia ni mwanasiasa makini. UKAWA ni muungano ambao hautaishia leo. Utakwenda hadi uchaguzi mkuu ujao, na ikibidi kuchukua Dola toka ccm.

2010 Mbatia aligombea jimbo la Kawe na kushindwa na Halima Mdee. Siamini kama 2015 atatamani kugombea urais. Wala siamini kama atakwenda tena kugombea Kawe kutokana na UKAWA. Kadhalika sina hakika kama ataenda kugombea jimbo la Vunjo ambalo akipata kuwa mwakilishi wake huko nyuma. Pale Vunjo yupo Mrema (wa chadema) ambaye aligombea na Mrema wa TLP na tlp ikashinda. Siamini kama nia za Mrema wa cdm zilifutika. Bila shaka atauwinda tena uwakilishi mwakani kwani Lyatonga sina hakika kama atagombea tena, au kupewa kura za kutosha kushinds.

Mbatia anahitajika mjengoni. Atapitia jimbo gani la uchaguzi?

Kwa Mbatia kuwatumikia wananchi si lazima awe mbunge. Kazi zake zinaonekana hata nje ya mbunge. Ndio maana hata mheshimiwa rais alimkubali na akamchagua, fikiria wana ccm wangapi mate yanawatoka!
 
Kule kwa Mtemvu mbona kunapitika kwa urahisi tu; atangaze nia!
 
The best alternative ni jimbo la VUNJO ambako aliwahi kuwa mbunge. Alibugi kwenda Kawe, Huyo Mrema wa CDM itabidi awe sacrificed, na hizo ndiyo cost za USHIRIKIANO WA VYAMA. They can learn from Kenya huwa wanafanya vipi.
Ni kweli mkuu. Hata mimi niliwaza Mrema kutoswa abakie mkurugenzi wa masuala ya bunge. Mbatia kugombea nje ya haya majimbo mawili haipendezi. Ni imani yetu hekima itatawala
 
Kwa Mbatia kuwatumikia wananchi si lazima awe mbunge. Kazi zake zinaonekana hata nje ya mbunge. Ndio maana hata mheshimiwa rais alimkubali na akamchagua, fikiria wana ccm wangapi mate yanawatoka!
Ni kweli lakini ubunge una nafasi kubwa sana kwenye suala la kufanya maamuzi
 
Kwani huu Ubunge ameugombea?

Hatagombea, Rais atakayepita atamchagua viti maalum.
 
Hatimaye naona kitendawili cha vigogo watatu wa jimbo la uchaguzi Vunjo chaanza kuteguka. Tusubirie yatakayojiri. Ila nisingependa kuona Mrema jr na Mbatia wakilumbana jimboni.
 
huyo Mrema Jr. 2010 performance yake ilikuwaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom