Baada ya U20 kuaibishwa kwa kichapo cha Mbwa mwizi huko Mauritania, Jamhuri Kihwelu afukuzwe haraka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,657
218,145
Hatuwezi kuwa na makocha wanaotegemea kukanyaga mafuta ili kupata ushindi , hii timu ya vijana sina hakika kama inaweza kupata hata goli kwenye michuano hii , achilia mbali kupata ushindi .

Jamhuri hana uwezo wowote ule wa kufundisha soka kwenye michuano ya kimataifa , hivi ni nani alimpa hii kazi ? hadi dk 90 Tanzania 0 - 4 Ghana

Napendekeza TAKUKURU kuchunguza kitengo cha ajira TFF
 
Tanzania hatuna vipaji vya mpira wa miguu, tunaupenda tu, lkn hakuna vipaji kabisa, mtalaumu makocha bure
Hapana kaka, mm nina experience ya soka la vijana.

Tatizo hao vijana wanachaguliwa kwa kujuana sababu nina vijana wadogo walikosa nafasi sababu hawana watu wa kuwashika mikono, wengine wameamua kuacha na mpira.

Tatzo kubwa ni TFF kuanzia ngazi ya chini mpaka juu
 
Hatuwezi kuwa na makocha wanaotegemea kukanyaga mafuta ili kupata ushindi , hii timu ya vijana sina hakika kama inaweza kupata hata goli kwenye michuano hii , achilia mbali kupata ushindi...
Kocha wa Uganda alishawahi kusema tatizo la Tanzania, badala ya kuwafundisha watu mpira, tunawajaza HAMASA! tukitegemea hamasa, tambo ndio zitatusaidia?!!ie tena huyo julio ndio hakuna kitu kabisa, yeye ni kulalamika tu, mambo ya nugaz, "AFE BEKI AFE KIPA HAWATOKI",

Hayo ndio huwa tunapenda kusikia!!mi nasema hivi soka limetukataa tuachane nalo tu, tufanye mengine" mala WADA!!!!Yaani utumie njia ile ile miaka nenda rudi halafu utegemee matokeo tofauti? Hata huyo Polsen walichomfukuzia miaka ile leo amerudishwa tena kuna mabadiriko yamefanyika ili yasiwe kikwazo tena kwake?!!
 
Walipokosea ni kumpa Julio timu kwa tunaomjua Julio huwezi kicheza bila kumpa asilimia kadhaa za posho kingine ili akuchague lazima umpe hela hivyo timu nzima inachaguliwa kwa rushwa wale wenye vipaji wengi huwa familia zao masikini
 
Hatuwezi kuwa na makocha wanaotegemea kukanyaga mafuta ili kupata ushindi , hii timu ya vijana sina hakika kama inaweza kupata hata goli kwenye michuano hii , achilia mbali kupata ushindi...
Mimi nashangaa hii timu kocha alikuwa zuberi katwila,ilikuwaje akapewa janhuri kihwelu?
 
Vijana wetu wamepangwa kundi gumu.

Ghana wametuacha mbali sana, kwa kichapo hicho nakiona cha kawaida tu.

Ila ni kweli Julio hakustahiki kukabidhiwa hii timu ya vijana.
 
Vijana wazuri Sana na wengi wanavipaji....tatizo hawana mbinu.... hawachezi kitimu....kila mtu yuko kivyake....wamekosa magoli zaidi ya matatu ya wazi....hawako makini katika ukabaji.....wamefungwa magoli mepesi Sana..... nadhani tatizo ni kocha.
 
Hatuwezi kuwa na makocha wanaotegemea kukanyaga mafuta ili kupata ushindi , hii timu ya vijana sina hakika kama inaweza kupata hata goli kwenye michuano hii , achilia mbali kupata ushindi .

Jamhuri hana uwezo wowote ule wa kufundisha soka kwenye michuano ya kimataifa , hivi ni nani alimpa hii kazi ? hadi dk 90 Tanzania 0 - 4 Ghana

Napendekeza TAKUKURU kuchunguza kitengo cha ajira TFF
CCM wame monopolize michezo, waachie gutimu gwao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom