kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,363
- 4,851
Wakuu kheri ya pasaka, juzi juzi mkuu wa baraza la usalama la urusi na rais mstaafu Dimitry Medved alionya kua endapo Finland na Sweden watalazimisha kujiunga Nato, basi urusi itakuja na jibu la nguvu sana ili kuleta balansi ya dunia.
Medved alisema watalazimika kupeleka majeshi na mitambo ya nyukilia kwenye mpaka wa Finland, itakumbukwa kua Finland na Russia wanashare mpaka mrefu wa kilomita 1300, umbali wa kutoka dar mpaka Bukoba. Na pia akasisitiza ukraine watapaswa kuishi na mizinga ya nyukilia karibu kitu ambacho hakijawahi kutokea.
Katika hali ya kupigilia "msumari wa moto" Medved alidai pia watapeleka ndege vita zenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyukilia, meli pamoja na wanajeshi ikiwemo mitambo ya ardhini ya nyukilia kwenye eneo lake la KALININGRAD lililopo kati kati ya Poland na lithunia. Wakifanya hivyo ina maana ulaya magharibi itakua na tishio la moja kwa moja la nyukilia kutoka Urusi. Swali ni je Ulaya itakubali hali hii kwa exchange ya Sweden na Finland kujiunga Nato?
Historia inatueleza bayana Russia alishawahi kua na mgogoro mkubwa wa kinyukilia na US mwaka 1960s, pale alipojenga mitambo ya nyukilia cuba pamoja na kusogeza nyambizi za nyukilia karibu kabisa na Marekani. Itakumbukwa kua mgogoro huu ulikua mkubwa sana tena sana mpaka wakafikia tamati ya mezani kupitia mkataba wa amani wa "CAMP DAVID PEACE ACCORDS "
Kwa jicho lako la kiuchambuzi na sio ushabiki, unadhani Finland na Sweden watakubaliwa Nato? Amani ya Dunia itakua kwenye hali gani ikiwa makombora ya nyukilia yakianza kuwekwa mipakani mwa nchi hasimu?
Nb: hapa chini nimeweka ramani ya ulaya, kuonesha eneo la urusi la KALININGRAD lililopo kati kati ya poland na lithunia karibu kabisa na Baltic sea. TUJADILI
The irreplaceable