Eng Nyahucho
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 688
- 1,152
KILIO CHA WATOTO WA MASKINI BAADA YA SERIKALI KUSEMA KUWA HAIAJIRI WALIMU WA MASOMO YA SANAA (ARTS)
Kwa kuwa watoto hawa wa maskini walikuwa na uhakika wa ajira baada ya kihitimu, na pengine wengine waliamua kuacha fani zao zilizokuwa damuni na zenye uwezekano wa kuwasaidia baadae hata kwa ku-hustle wakaamua kusomea uwalimu kwa sababu serikali iliwahakikishia mkopo na ajira, ni bora ifikirie upya namna ya kurudisha matumaini yao ili na serikali ipate kulipwa mkopo iliyowakopesha.
Sio lazima sana kuwaajili kama serikali haina uhitaji wa walimu, ila serikali ina uwezo wa kuwaajiri ktk sector zingine maana taaluma ya uwalimu ni pana zaidi.
Kwa wale watakaohitajika kuwa na ujuzi maalum serikali inaweza kuwapangia mafunzo maalum ili kuendana na hitaji la soko.
Mheshimiwa Rais kama anavyosema na kutenda kwa ajili ya watanzania maskini, na zaidi ya 80% ya walimu hawa wa masomo ya Arts wanatokea familia maskini ni vyema akalifikiria tabaka hili pia.
Naandika haya sio kama nimetulia sana kiakili kwa kuwa nami ni muhanga wa hili wala sio kwamba nimepumzika sina kazi ya kufanya la!
Naandika haraka haraka ili nisimuangushe Rais wangu kwa slogan yetu ya "Hapa Kazi Tu" hivyo mawazo haya kama hayajakaa vizuri sana yasichukuliwe kama mawazo ya mjinga bali kama mawazo ya mtu aliyekata tamaa.
Najua Mheshimiwa hayumo kwenye kundi hili lakini wateule wake kuanzia Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi, Ma-RAS na Ma-DAS pia viongozi waandamizi wa chama wamo humu watamfikishia kilio hiki.
Kumbuka kusoma ni kuwekeza. Tuliwekeza zaidi ya miaka 20 na kwa bahati mbaya product yetu ya mwisho tuliyotoa ni Elimu!
Mkituacha ni sawa na kutuchimbia kaburi maana hatuna pengine pa kupata soko la bidhaa hii.
Imeandikwa na;
Marwa Charles
"Mtoto wa mkulima jembe la mkono"
Kutoka kijiji cha Keisangora Kata ya Nyamwaga Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.
0767 35 45 55