Baada ya Mungu ni mzungu

Baada ya Mungu ni mzungu

OR Recipe

Senior Member
Joined
Jul 2, 2014
Posts
150
Reaction score
34
Siku zote katika maisha yangu huwa cpendi kujishusha hadhi kwa binadamu mwenzangu ambaye anaroho kama yangu. Ninasema hivyo baada ya kusikiliza wimbo wa msaani NIKI WA PILI katika wimbo wake wa staki kazi. Moja kati ya verse yake aliyosema "BAADA YA MUNGU NI MZUNGU hii kwangu naona NIKI yeye kama yeye kajidharau sana mbele ya hawa watu weupe. Kwani mzungu sio binadamu kama watu wengine?
 
tusubiri mvua za matusi...
 
kwan hata ktk uhalisia iko vp hebu jaribu kwanza kushindana na mzungu kwenye nyanja mbalimbal za kimaisha halafu uje utupe mrejesho hapa!
 
Muingereza anang'aa na vito vya dhahabu kuliko mbongo wakati ardhi ya bongo ina dhahabu kuliko uingereza, utamueleza nini mzungu wewe!
 
Dogo kaimba vizuri tu, kinyume na hapo basi ni kujitutumua kusiko na faida yoyote
 
Siku zote katika maisha yangu huwa cpendi kujishusha hadhi kwa binadamu mwenzangu ambaye anaroho kama yangu. Ninasema hivyo baada ya kusikiliza wimbo wa msaani NIKI WA PILI katika wimbo wake wa staki kazi. Moja kati ya verse yake aliyosema "BAADA YA MUNGU NI MZUNGU hii kwangu naona NIKI yeye kama yeye kajidharau sana mbele ya hawa watu weupe. Kwani mzungu sio binadamu kama watu wengine?

Ndio ukweli, unauma najua. Waafrika bado sana. A simple example: Nambie any scientific discovery ambayo ni nguzo ya dunia ambayo imefanywa na mwafrika. Tazama ebola, tangu 1976 iligunduliwa Congo na mzungu-just imagine mpaka leo Congo or any other African country hakuna research ya "maana" iliyofanyika kuhusu ugonjwa huo ukiacha prevalence (watafiti wananielewa)
 
Ndio ukweli, unauma najua. Waafrika bado sana. A simple example: Nambie any scientific discovery ambayo ni nguzo ya dunia ambayo imefanywa na mwafrika. Tazama ebola, tangu 1976 iligunduliwa Congo na mzungu-just imagine mpaka leo Congo or any other African country hakuna research ya "maana" iliyofanyika kuhusu ugonjwa huo ukiacha prevalence (watafiti wananielewa)

Ni utumwa fikra tu. Mie nimekaa na kuishi nao. Sema wanajua vitu vingi sana. Wakti sisi bado tumelala.
 
Ni utumwa fikra tu. Mie nimekaa na kuishi nao. Sema wanajua vitu vingi sana. Wakti sisi bado tumelala.


Umeshaandika sisi bado tumelala.... Na wao wanajua vitu vingi sana, Sasa iweje
Uone ni utumwa wa fikra!?
 
Ni utumwa fikra tu. Mie nimekaa na kuishi nao. Sema wanajua vitu vingi sana. Wakti sisi bado tumelala.



Lengo lako ni kutuhabarisha kwamba umekaa na wazungu... Heko mkuu
 
YESU KRISTO NI MUNGU !
sifa na utukufu apewe yeye tu !
LICHA YA BIBLIA KUTWAMBIA WAZI WAZI KUWA YESU NI MUNGU !
Katika Biblia neno Bwana/ BWANA hurejerea Mungu/MUNGU !

sasa Leo tunaona namna ambavyo Yesu Kristo ndiye MUNGU, kwa kulichunguza hili jina " Bwana "

"Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine ; zaidi ya mimi hapana Mungu " ( Isaya 45:5).
Bwana ni Mungu !
Kipindi waisraeli wakiteswa huko utumwani misri , aliyekuja kuwaokoa bado alikuwa YESU huyo huyo ambaye ndiye Bwana !
" Bwana akasema , Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko misri , nami nimesikia kilo chao kwa sababu ya wasimamizi wao ; maana nayajua maumivu yao"
( kutoka 3:7).
Lakini Musa alitaka kumkwepa Bwana kwa kusema kuwa eti yeye si mfasaha wa kusema , kwahiyo asitumwe yeye kwenda kuwatoa waisraeli huko misri mbele ya farao.
Lakini :
" Bwana akamwambia, Ninani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu ?Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi , au Mwenye kuona au kuwa kipofu? Si Mimi , Bwana ?
( kutoka 4:11).
Bwana ndiye muumbaji !
Basi hata hivyo Musa alikuwa ameuliza jina la huyo Mungu ni lipi;
" Mungu akamwambia Musa , MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema , ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli ; MIMI NIKO amenituma kwenu"( kutoka 3:14).
YESU alipokuwa hapa duniani alijitaja wazi kuwa yeye ndiye " MIMI NIKO " mbele za wayahudi.
" Yesu akawaambia, Amin , Amin nawaambia, yeye Ibrahimu asijakuwako , Mimi Niko "
( Yohana 8:58)..
Huo ulikuwa ushuhuda kuwa yeye ndiye yule waliyemsikia akinenwa ndani ya Vitabu walivyokuwa navyo;
YESU aliwaambia wayahudi kuwa maandiko yote wanayoyasoma yanamshuhudia yeye YESU, yaani maandiko yote yanatoa sifa na ukufufu wa Yesu Kristo AMBAYE ndiye Mungu aliyejidhihirisha wazi katika mwili.
" Mwayachunguza maandiko , kwa sababu mnadhani ninyi mna uzima wa milele ndani yake ; na hayo ndiyo yanayonishuhudia "( Yohana 5:39).
Lakini hapa pia baada ya wana wa Israeli walipoyashuhudia mambo makuu ya Bwana kwa kuwatupa wamisri baharini , WALIMWAMINI BWANA, WAKAMCHA BWANA , NA Musa mtumishi wake ( kutoka 14:31)
Wakasema haya ;
"Bwana ni mtu wa vita , Bwana ndilo jina lake "( kutoka 15:3).
Sasa ;
Yesu Kristo alikubali HADHARANI KUWA YEYE NDIYE Bwana (siyo bwana maana bwana ni yeyote yule hata mimi ni bwana ) LAKINI Bwana/ BWANA ni jina ambalo hupewa MUNGU Pekee .
" Ninyi mwaniita , Mwalimu , na Bwana ; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo"
( Yohana 13:13).
Yesu ndiye Bwana yaani ndiye Mungu.
Wana wa Israeli walisema wanatoka misri ili wakamtumikie Bwana , Mungu ;
" La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani , tumchinjie dhabihu Bwana , Mungu wetu kama atakavyotuagiza"
( kutoka 8:27).
Ndugu ;
Bado hili jina Bwana ni la Mungu mwenyewe , YESU ni Mungu.
Baadaye katika safari ya wana wa Israeli kutoka utumwani misri , Bwana hakupenda watu wake waishi kama walivyokuwa wanaishi huko misri , aliwapa sheria zake ili ziwaongoze namna ya kuishi wao kwa wao na namna ya kumtumikia Bwana Mungu.
Alianza kwa kujitaja kuwa yeye ni Bwana , Mungu wetu ;
"Mimi ni Bwana , Mungu wako , niliyekutoa katika nchi ya utumwa,usiwe na miungu mingine ila Mimi" ( kutoka 20:2). Endelea mpaka msitari wa 17 amri kumi alizitoa Bwana.
Sasa,
Huyu MUNGU wetu baada ya kuona kuwa wanadamu tumetenda dhambi na tunakabiliwa na kifo , aliamua yeye mwenyewe kujitoa kwa ajili yetu ili tusife milele
( Yohana 3:16).
NDUGU YANGU !
Kwa YESU kila goti litapigwa ,na
kila ulimi utakiri , Yakuwa KRISTO NI Bwana , kwa utukufu wa MUNGU Baba, hata waliomchukia watampigia Magoti kwa kutahayari na kutetemeka huku wakikiri KRISTO NI BWANA ( Flipi 2:11)
& Isaya 45:23-24.
Sasa huyu Bwana ndiye anayeumba mbingu mpya na nchi mpya ambapo wanadamu wote watakwenda mbele zake kuabudu kila siku ya sabato;
"22.Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ,nitakazofanya , zitakavyokaa mbele zangu , asema Bwana , ndivyo uzao wenu utakavyokaa.
23. Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya , na sabato hata sabato , wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu asema Bwana "
(Isaya 66:22-23)..
Na siku ya Bwana :
" Bwana atakuwa Mwenye kuwatisha sana; kwa maana atawasafisha kwa njaa miungu yote ya dunia ; na watu watamsujudia yeye , kila mtu toka Mahali pake ; nchi zote za mataifa"
( sefania 2:11).
NDUGU YANGU YESU KRISTO NDIYE MUNGU AKIWAKILISHA UTATU MTAKATIFU.
"Kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni , Baba , na Mwana , na Roho Mtakatifu , na watatu hawa ni umoja "(1yohana 5:8)
Amua kuwa upande wake !
BWANA Awabariki



jifunze:horn:
 
  • Thanks
Reactions: J C
Koma ww bila mwafrica hakuna mzunguu nyooo na hii mimali yetu na material yetu wanavotegemea nyambavu kasoro mkia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom