Buenos Aires
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 1,894
- 1,622
BuenosAires,Argentina.
BAADA ya Lionel Messi kutangaza kustaafu kuichezea Argentina watu mbalimbali wamejaribu kuonyesha ni jinsi gani taifa hilo la Amerika ya Kusini litapoteza kitu muhimu nje na ndani ya uwanja hasa Matokeo,Mapato pamoja na Mvuto. Soka Extra inakuletea kile kilichosemwa na Guillermo Tofoni,ambaye ni Mratibu wa Mechi zilizo chini ya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA,kufuatia Messi kujiengua Kuichezea Argentina. Tofoni amejaribu kujikita zaidi katika suala zima la hasara ambazo Argentina itakumbana nazo katika kipindi chote ambacho haitakuwa na Mshindi huyo mara tano wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia. Tofoni amesema "Ikiwa Messi hatarejea kuichezea Argentina,chama cha soka cha nchi hiyo,AFA, kitapata hasara ya kati ya Dola Milioni 20 mpaka Milioni 25 ama zaidi ya hapo,kuanzia sasa mpaka kufikia kombe la dunia la mwaka 2018. Hasara hiyo inatarajiwa kuwa kubwa zaidi mpaka kufikia Fainali za Kombe la Dunia la Mwaka 2022, ambazo zilitarajiwa kuwa za mwisho kwa Messi. Tofoni amesema tayari Mataifa kama Italia,Hispania na China yameshaanza kufanya nae mawasiliano tangu Messi alipotangaza kustaafu kuichezea Argentina mwezi uliopita yakitaka kufanyike marekebisho ya gharama za malipo za kucheza na Argentina isiyo na Messi. Tayari Urusi imeshasema itapunguza kiwango cha pesa kwa Argentina kwa kiasi cha Dola Milioni 1 kama malipo ya mchezo wao wa kirafiki utakaochezwa Juni 2017 ikiwa Messi hatakuwa amerejea mpaka wakati huo.Amesema Tofoni. Kwa kawaida Argentina huwa inalipwa mpaka kufikia Dola Milioni 2 kucheza mchezo mmoja wa kirafiki ikiwa na Messi kikosini. Tofoni ameendelea kutanabaisha kuwa Argentina inatarajiwa kucheza takribani michezo 28 ya kirafiki kabla ya mwaka 2022 hali ambayo itapunguza mauzo ya tiketi kwa kiasi kikubwa ikiwa Messi hatakuwepo. Kati ya michezo hiyo 28,michezo 16 imepangwa kuchezwa nchini Argentina.Kwa mujibu wa Tofoni hii ina maana kwamba Argentina itapata hasara ya Dola Milioni 1 katika mauzo ya tiketi kwa kila mchezo itakaocheza nyumbani bila ya kuwa na Messi kikosini. Hasara hiyo inatarajiwa kuwa itaongezeka na kufikia mpaka Dola Milioni 16 mpaka kufikia Kombe la Dunia la mwaka 2022 litakalofanyika huko nchini Qatar.