Baada ya Lissu kuchukua fomu ya Urais, Dr Mwakyembe atishia kuifuta TLS

Status
Not open for further replies.

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Kuna nini nyuma ya kauli hii ya Mwakyembe kutaka kufuta chama TLS? nahisi sababu ni Lissu kugombea uenyekiti
yetu macho

imag1e-jpeg.470937

Chanzo Azam two

Baada ya Tundu Lissu na Law Masha kuchukua form za kugombea uongozi wa Tanganyika Law Society,Waziri wa Katiba na Sheria Dr Mwakyembe,amesema wataifungia TLS na kumuomba msajili wa vyama vya siasa Jaji Mtungi aisajili kama Chama cha Siasa.

Kupitia Azam Two,Dr H.Mwakyembe anasema,endapo vuguvugu hilo la wanasiasa wa chama fulani watafanikiwa kushinda na kuiongoza TLS,basi Wizara yake itapeleka bungeni hoja ya kuifuta sheria iliyoanzisha Tanganyika Lawa Society na hivyo kuiondoa na kuacha ibaki kama NGO.

Hivyo amewaonya mawakili kutokukubali kuiingiza TLS kuwa kama chama cha siasa,ama wakubali ifutwe au iendelee kuwepo kama taasisi inayosimamia mambo ya sheria na uweledi wa wanasheria Tanzania.

Dr Mwakyembe amesema,Serikali ya awamu ya tano haiana bla bla na mizunguko,itakalolisema ndio inalolitenda,hivyo kama TLS hawatazingatia,basi serikali haitasita kuifuta na kuiondoa kabisa.
Cc: Petro E. Mselewa
-------
"Serikali imekiasa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kibaki kuwa chombo cha kitaaluma cha kulinda weledi, viwango na maslahi mapana ya uanasheria na kisikubali kuyumbishwa na mihemko ya uanaharakati wa kisiasa isiyo na tija kitaaluma.

Akiongea na ujumbe wa TLS kwenye ofisini yake ndogo ya Dar es Salaam leo, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema TLS ibakie njia kuu kama ilivyo kwa vyama vingine vya kitaaluma nchini, isighilibiwe na michepuko.

Amesema uanzishaji na uendeshaji wa TLS kwa sheria ya Bunge umesukumwa miaka yote na dhamira njema ya Serikali ya kutaka kuilinda na kuilea taaluma ya uanasheria ili ikue na ijenge weledi stahili na hivyo itoe mchango bora katika ujenzi na uendeshaji wa utawala wa sheria nchini.

"Ikiwa TLS sasa inajiona imekua kiasi cha kutosha na sasa inataka iingie kwenye majukumu ya ziada ya uanaharakati wa kisiasa, Serikali haitasita kuifuta sheria iliyoanzisha TLS ili chama hicho kijisajili chini ya Sheria ya Vyama kama NGOs zingine nchini au ikiwezekana chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa kama vyama vingine vya siasa nchini".

Ameongeza kusema harakati zinazoendelea ndani ya TLS zenye mwelekeo wa kisiasa, zimeifanya ofisi yangu isimame kidogo kukamilisha marekebisho kadhaa ya sheria ya TLS maana hatma ya TLS haieleweki, "it remains in the balance".

Awali, waziri huyo aliueleza ujumbe huo wa TLS ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TLS, Wakili Lameck Calleb, kuwa Serikali imefarijika sana kwa ushirikiano mkubwa uliotolewa na chama hicho katika maandalizi ya muswada wa sheria ya huduma ya msaada wa kisheria ambayo imepitishwa na Bunge na sasa unasubiri saini ya Rais wa Nchi kuwa sheria.

Aliongeza kuwa Wizara inaitegemea sana ushurikiano wa TLS hata katika utungaji wa Kanuni za sheria hiyo mpya, mchakato wake ambao tayari umeanza."
 
imag1e.jpeg
View attachment 470935 View attachment 470936 Baada ya Tundu Lissu na Law Masha kuchukua form za kugombea uongozi wa Tanganyika Law Society,Waziri wa Katiba na Sheria Dr Mwakyembe,amesema wataifungia TLS na kumuomba msajili wa vyama vya siasa Jaji Mtungi aisajili kama Chama cha Siasa.

Kupitia Azam Two,Dr H.Mwakyembe anasema,endapo vuguvugu hilo la wanasiasa wa chama fulani watafanikiwa kushinda na kuiongoza TLS,basi Wizara yake itapeleka bungeni hoja ya kuifuta sheria iliyoanzisha Tanganyika Lawa Society na hivyo kuiondoa na kuacha ibaki kama NGO.

Hivyo amewaonya mawakili kutokukubali kuiingiza TLS kuwa kama chama cha siasa,ama wakubali ifutwe au iendelee kuwepo kama taasisi inayosimamia mambo ya sheria na uweledi wa wanasheria Tanzania.

Dr Mwakyembe amesema,Serikali ya awamu ya tano haiana bla bla na mizunguko,itakalolisema ndio inalolitenda,hivyo kama TLS hawatazingatia,basi serikali haitasita kuifuta na kuiondoa kabisa.
Cc: Petro E. Mselewa
 
Hats Mimi ningeifuta au iwe chama cha siasa

Tusiishie hapo Tufute na Chama Cha Walimu, Chama cha Wakulima, Chama Cha Waganga, Chama Wahasibu, Chama Cha Madaktari, na vyama vyote vinavyofanana na hivyo.


Hiki kichwa kinawaumiza sana vichwa awamu hii, uzuri wake hakiteteleki na kurudi nyuma.

Nilishawahi sema akinyamaza TL nchi hii basi tumekwisha maana wasomi na vyombo vya habari vimeshasarenda.

Viva Tundu Lisu.
 
Hayo yamesemwa na waziri wa sheria na katiba mhe, Harrison Mwakyembe

Source....Azam news
42feae30b2b01dc9197c5b4dda50b084.jpg

Sababu kuu aliyo isema waziri
Ni siasa ya vyama ndani ya TLS
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom