IBRA wa PILI
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 1,549
- 2,668
Akuna muda wa kupoteza
Tuendelee Sasa
Baada ya kurudi hapa tz nyumban nikiwa mfukoni Nina elf 30 TU naikimbuka sana hii siku nikawasili maskani ikiwa saa 3 usiku wife akuamka sio ishu ya chakula Wala kuweka maji ya kuoga na alinisikia nikifika ila mlango alifungua mtu mwingine.
Nikaweka beg langu uzuri nilisha kula stend mgahawan so sikuuliza nikaona ajiangaishi na chochote mi nikalala zangu hapo nikawa na mawazo chungu nzima naanzaje life.
Hapa machalii wapo wawili na kule Mozambique mambo yalienda ndivyo sivyo ila pesa kwa wife nilikua natuma sana,
nilipunguza kutuma baada ya kupata shoti kwenye Kaz yangu ambayo nilikua nafanya ya kununua dhahabu na ndio ilipelekea mpaka nikaludi nyumban nikiwa Sina kitu.
Asubuhi wife alikua wa kwanza kuamka akafanya shughuli zake alipomaliza akaenda kwenye mishe zake na hata akuniaga mi pia Nika amka nikafanya mambo yangu nikasepa kitaa.
Jioni aliporudi Yuko bize na mambo yake mpaka nikajiuliza uyu mtu kapatwa na nini Yani ni kama nilikuepo tu hapa na sijatoka mahali nikamuuliza toka nimerudi upo bize ni kama unioni kwani vipi akajibu we unayo Fanya uyaoni, nikamuuliza yapi ayo akajibu mkato mi sijui unajua mwenyew, nikamwambia kwaiyo utaendelea kua bize ivyo ivyo akajibu ndio nikasema sawa watoto si hawa hapa acha tupambanie watoto basi akuna shida we endelea kua bize akasema sawa.
Niliwaza sana pesa nilikua natuma ya matumizi alafu naludi naonekana kama nilijizila huko niliko au kama nilikua sikumbuki familia afu nikiyumba ndio inakua shida kwa wife.
wakati nakaribia kuludi ndio nikapata shoti sasa baada ya kupata shoti nilikua natuma pesa lakini ndogo tofauti na mwanzo nikaona shida ndio iliko anzia.
Ok Nika endelea ku unga unga kitaa na washkaji sometimes nikipata vijisent huko maisha yanasonga wife Yuko bize sikujali sababu niliona kashahamua kua ivyo ila Nilijua Kuna kidudu mtu kimeingia hapa sio bule
yeye alikua anafanya biashara ya dagaa Sasa huko kwenye biashara Kuna mengi marafiki wa ovyo wazuri pia wapo, vishawishi vingi n.k.
Hapo ilikua ni mwaka 2022 mwishoni Yani mwez wa 12 mshikaji wangu yule wa MSUMBIJI alisema tuonane tukakutana kwenye pub maarufu sana pale songea
LA CHALZ.
tukapiga stor sana zaidi alisema mwanang sitakutupa japo ulipata shoti ila mambo acha yakae sawa tutajua tunafanya Nini yeye alikua anakunywa bia safari mi nilikua napiga Pepsi wakati tuna endelea na maongezi akapita demu flani hivi tulikuaga nae huko msumbiji akajiunga bana stor mbili tatu wakaeleewana waende gest apo ni saa saba usiku.
Akaniambia nimsubiri pale wakaenda huko gest zimejaa zingine zimefungwa wakarudi pale jamaa akasema ngoja naenda kupiga mpenyoni uyu waka ondoka Tena baada ya robo saa wakarudi😄😄 jamaa akasema uhakika kapiga
, stor zikasonga baadae demu akaanza kudai ela jamaa akazama mfukoni akatoa elfu kumi akampa demu akasepa si tukaendelea pale mpaka saa 8 hivi tukatoka mshkaj akachukua boda mi akanipa buku 2 mhm niliguna moyoni ye akachukua boda tukaagana aka enda mi nikatoka mdogo mdogo ule usiku na Giza mpaka home sikupanda pkpk nafika maskani saa9 nikazama ndani kimya kimya tu wife alifungua mlango.
Tupo ndani wife akasema kwaiyo saiz ndio umeamua kuludi usiku namna hii nikamwambia hata nikiwai, niwai Nini si Kila mtu yupo bize Kuna tatizo na je kama nafanya kazi, akasema naomba iyo ela uliopata huko kazini nikamwambia kama nalipwa kwa wiki au mwezi nikamwambia alafu usinipande kichwani we uko bize endelea kua bize.
Asubuhi maisha yakasonga ubize kama kawaida Kuna mshkaj wangu alikua anasimamia tofali za bloku Kijiji flani hivi akaniambia kama vipi twenzetu mwanang tukapige kazi nikaona nifanye ivyo.
Iyo siku nikachukua godoro la kulalia na nguo zangu chache asubuhi wife nikamuaga Kuna sehemu naenda Fanya Kaz akajbu sawa akuuliz Tena chochote labda Kaz Gani, unaludi lini je malipo yake akuna alafu kumhaga upande wangu ilikua kutafuta amani niendako ila niliona akuna amani kwa alivyojibu.
mi nikasepa na mshikaji mpaka maeneo ya kazi tulienda na gari. So tulifika ile siku kama mida ya saa moja hivi tukaenda tafuta mgahawa tukala msosi fresh stor nyingi cheki mazngira maana mi ndio nilikua mgeni pale.
Siku ya pili asubuhi wakati tunataka kuanza kazi machine ya kuchanganyia mchanga na cement ikazngua ikabidi mpaka aje fundi kutengeneza baada ya kukaa sawa machine usiku hivi tukaanza kazi kama nusu saa ilitosha machine ikabuma Tena na kazi ikaishia hapo tukaenda kulala ili asubuhi mafundi waje Tena kurekebisha.
Asubuhi na mshkaj baada ya kupata chai tukawa tuna zurula TU tukisubiri mafundi na boss alivyofika akaja na wazee flani hivi ili kupiga ndagu pale maana alihisi anafanyiwa mchezo so akachinjwa mbuzi na maseke mengne kibao kwenda kuchimbia kwenye machine sjui ngozi na makolokolo mengne.
Sku ya pili baada ya kuweka fresh machine kazi ikaanza baadae ikaja Dili ya kupakia tofali kwenye Gari nikajiunga chapu na Mimi kupakia tukiwa tunapakia pale tofali wakati naweka tofali kwenye Gari Kuna jamaa tofali ilimtoka mkononi ikanigonga Mimi mkono wa kushoto nikaumia na kazi ikaishia hapo.
Nilikaa pale siku kama mbili hivi sjapona mkono, nilichua na dawa flani hivi alafu nikafunga na bandeji mkononi ikabidi nifanye mpango wa kusepa tu Sasa wife nikampa taarifa kwamba nimeumia jibu likawa sawa akutaka kujua ilikuaje na nimechukua hatua Gani akuna sikujali nikaludi home 🏠.
Kabla ya kufika nyumban nikapita sehemu flani hivi Kuna wi-fi ya kitonga nikatulia pale nikaperuz mpaka mida ya saa mbili nikaenda maskani, kufika pale home nikamsalimia wife Cha kwanza kwake akauliza ela uliopata huko ikwapi ?!
Nikamwambia ndio Cha kwanza kuuliza hicho nilikupa taarifa nimeumia uhulizi afya yangu unauliza pesa we ni mtu Gani ujali afya ya mwenzio Ivi bila afya njema iyo pesa natoa wapi we mpumbavu unaweza pesa kuliko Hutu hapo alikaa kimya na angeendelea ningempa viganja aliniboa sana.
Siku ya pili au ya tatu toka niludi kule kwenye tofali mama yangu mkubwa ana guest na grocery eneo flani hivi akaniambia nikamsaidie kusimamia angalau nikapata sehemu ya kupotezea muda na kupata vijisent siku nyingne nikawa nalala huko nikachukua na nguo chache fresh ikawa nikipga hesabu pesa kidogo napeleka home, lakini hapo nikawa nawaza nipate mishe ya maana ya kufanya na sio kutegemea pale.
Bana bana bana wife akiwa huko na wenzake akatangaza nyumban pale nimehama aisee na sikumwambia nalala wapi na nimepata ka kibarua wapi kwasababu hata nikimwambia ajali chochote nikaamua kukaa kimya tu ndio akatangaza nyumban pale nimehama akikutana na jamaa zangu maneno ndio ayo.
Sikujali Mimi nikaendelea pale na ile kazi Kuna siku nikawasiliana na mshikaji wangu mmoja alikua pwani Dar kwenye kiwanda anafanya kazi kiwanda Cha Tiles (malumalu) nikamwambia anifanyie mpango na Mimi niende kupiga kazi akasema nijipange ye anaweka michongo fresh niwe na nida, tin number kwajili ya nssf na nifungue account nmb.
Akasema ana mpanga kiongozi niandae 50 nikasema poa nikajichanga chap nikapata nauli na iyo 50 ya kumpa kiongozi aongee na meneja Nika mtel na bi mkubwa nae akaniongezea pesa safari ikakamilika wazee.
Nida nilikua nayo tin number nikaenda website ya Tra chap nikapata tin number, akaunt sikufungua jamaa akasema ntafungua Kule pwani nikifika.
Kesho kutwa safari Leo nikaenda hom bana sikukuta funguo inapokaa ili niweke mazngira fresh ya kuondoka nikamcheki wife kwa simu akaniambia unataka Nini hapo nyumban we si umehama nikamwambia nilikwambia nimehama lini mbona nguo zangu na vitu vyangu vipo ndani niambie funguo ipo wapi
Nataka Kuingia ndani gari inanisubiri natak kuondoka Nika mzingua una nichelewwsha ujue funguo inakaa nyumbani je ukipoteza huko ulikobeba nataka funguo Sasa hivi nikija huko ulipo ukorofi.
Akasema mi nipo mbali na funguo Kuna mtu nime muachia nikamuuliza umeenda wapi na kwann funguo umkabizi mtu ilikua na maana Gani we kuibeba huko nikamwambia naondoka endelea na mambo Yako gari nishachelewa nikasepa.
Siku ya pili asubuhi nikaenda maskani sikua na stor nyingi kwake nikampa elfu kumi kwanza nikanunua dagaa dumla moja kwake hapo nilikua na mafuta ya kula alizet pamoja na unga ili nikifika kwa washkaji nisiwe mzigo,
Baadae nikamuachia pesa ya matumizi.
Hapo nilikua nakopaga hela pesa x nilifikisha EF 50 nikakopa hii niliwapiga sikuwai kulipa mpaka Leo hii,
ila walisumbua sana na bahat mbaya niliweka namba ya broo wakawa Wana msumbua kinoma.
Ilikua ni mwezi wa tatu iyo ya mwaka 2023 tarehe sikumbuki.
Siku iliwadia wife nilimuhaga jibu ni sawa akuuliza chochote huko niendako na akuwai kuuliza, na hata akujua naenda Fanya kazi gani
Asubuhi ya saa kumi na moja siku ya pili ake nilipanda selous express na saa kumi na mbili chuma ilianza safari kuelekea pwani
Hapa Sasa ni maisha mengine mapya ya kazi niendako ni Pwani, Dar es Salaam najua ni mikoa miwili tofauti ila pwani ziko nyingi Sasa hii ni Pwani ya Dar wilaya ya kibiti sijui ni mkuranga nafikiri msha elewa......
Tukutane baadae tukijaaliwa tuendelee nilipo ishia chiiiiiiiaaaziii
(Tusamehane uandishi)