Katika mkutano wa kijiji jamaa akaibuka ghafla na kukatisha hotuba ya mwenyekiti, mkononi ana bonge la shoka huku akisema "nasikia nilipokuwa jela kwa miaka mi5 kuna jamaa alikuwa ananitafunia mke wangu, siwezi kuishi tena uraiani, hii ni aibu kubwa kwangu, mbaya wangu yupo ndani ya hili kundi na ni bora nimmalize kwa hili shoka nirudi jela.
Jamaa akaanza kupiga hatua kuifuata halaiki iliyoko mbele yake akiwa na shoka mkononi. Jamaa alizimia kwa kile alichokishuhudia, walitimka watu 10, miongoni mwao ni baba yake mzazi, mdogo wake na mwenyekiti wa kijiji.