Baada ya kutimuliwa mawaziri, nimeichukia zaidi CCM Sababu ni hizi:-

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,120
2,000
Baada ya shinikizo kubwa la bunge lililosababisha rais kutokuwa na uchaguzi zaidi ya kuwafuta kazi mawaziri wanne, kumekuwepo na juhudi zisizo za kibinadamu kuwasafisha mawaziri hao na kufunika kilichofanyika chini ya wizara zao.

Leo katika gazeti la mwananchi wameandika eti wasomi wanajadili jinsi mawziri jinsi wanavyoweza kugombea urais! Hivi Ccm kwao urais ni kitu cha muhimu kuliko maisha ya watu? Mbona hatusikii mijadala kuhusu vifo vya watu waliokufa kwa usimamizi wa watumishi wa wizara hizo?

Mbona hatusikii mijadala na mashinikizo ya wajane na yatima wahanga wa mauaji kulipwa fidia? Mbona hatusikii majeruhi wakiandaliwa safari za India na A. kusini kutibiwa? Mnadhani watanzania ni wapumbavu kiasi hicho, mmuwaue wengine wabaki vilema alafu mje kuchukua kura zao!

Ama kweli Ccm ni chama cha mizigo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom