Baada ya kutemwa, Adebayor aenda Crystal Palace

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
39,981
96,231
Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo aliyewahi kuichezea vilabu vya Arsenal, Man City na baadae Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor alikuwa hana timu kwa miezi kadhaa sasa baada ya kocha wa klabu yake ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kumuondoa katika mipango na kikosi chake kitakachoshiriki mashindano tofauti, licha ya kuwa alikuwa analipwa kama kawaida.

January 26 mitandao ya soka ya Uingereza imethibitisha Adebayor kujiunga na klabu ya Crystal Palace ya Uingereza, licha ya kuwa Crystal Palace na Adebayo hawajaweka wazi au kuthibitisha dili hilo, Sky Sport wamethibitisha staa huyo kujiunga na klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom