Baadhi ya vioo vya OLED vinakua na PWM (Pulse-width modulation) flickering. Vioo vya vya electronic devices vinatumia PWM kucontrol brightness ambapo kinakua kina switch ON and OFF kwa haraka sana. Ssa kuna baadhi ya watu (kama wewe) wanakua wapo sensitive sana na hii ON & OFF kiasi cha kwamba unakua unaona kma display ina cheza cheza. Kwenye OLED ni vigumu kuona display inacheza cheza ila inakua inakuumiza macho na kichwa. Kwenye LCD ndio utaona inacheza cheza. Mara nyingi simu za bei rahisi ndio zinakua na hili tatizo, unakua unaona kma mwanga kwenye kioo unacheza cheza.
Ushauri ni kwamba usipunguze brightness mpka chini au mpaka juu ukiwa unatumia simu ndani au usiku. Tumia brightness ya wastani tu