Baada ya Kurudishwa Kutoka Marekani.


Nashukuru sana kwa ushauri mzuri mkuu. Ntafikisha ujumbe!
 

Nakubaliana na wewe. Tukipata nafasi tuzitumie vizuri na kuinvest kwenye vitu vinavyo appreciate in value over time.
 

Umenena Ukweli Mkuu Asante!
 
Hivi 'elimu' ni nini? Inapatikana wapi? Uzoefu unaweza 'unaelimisha'?
Swali zuri, naomba nikupe maoni yangu
Kufanikiwa maishani unatakiwa uwe na akili. Wengi wenye akili nyingi wana elimu ya juu, ingawa siyo wote.
Mleta mada, nadhani alikuwa hajui tofauti ya kuwa na akili na kuwa na elimu ... nawajua wasomi wengi bongo ambao wanatia huruma na wasio wasomi hapa US ambao wanapeta.
Ukiamua kuparty bila kuinvest, hata kama una elimu gani, hiyo si akili nzuri. Ukiamua kuinvest na kufanya kazi kwa bidii, hata ukiwa fundi seremala, au fundi matope bongo utafanikiwa kama una akili.
 
Reactions: SMU
Yooote tuandike hapa....Lakini cha msingi hawa jamaa wanahitaji msaada. Umeshapanga namna ya kuwasaidia hawa rafiki zako. Tuache blah blah wakati watu wana shida.
utamsaidia mtubmwenye umri wa 45? Unajua midlife crisis wewe? Acha kabisa aisee.
 
Mwanangu Money Stunna acha visingizio. Kwani unadhani ni wewe pekee uliyeishi Marekani? Mbona tupo wengi na tumesoma na kusomesha? Tafuta sababu nyingine. Kama umejipanga vizuri ni rahisi kusoma Marekani kuliko Bongo. Hivyo mwanangu jiangalie upya ubadili mikakati utasoma tu kama una nia ya kufanya hivyo hasa ukizingatia umuhimu wa kufanya hivyo.Nadhani hii itakusaidia kubadilisha perception yako juu ya hili.
 

ndio unaweza kujisomesha sijakataa,lakin kwa vijana wengi inakuwa ngumu,mtu anasoma mwaka wa kwanza harafu anabez kwenye kazi anaacha,matumiz yanakuwa makubwa sana,asa kama hauna ndugu wa kukusapoti,bill zinakuwa nyingi,unaona ufanye full time job,vijana wengi inawashinda mkuu,mim nasemea kitu ninachoona si kuambiwa
 
Mwanangu Money Stunna umesema vyema. Hapa tatizo si Marekani bali mipango ya mtu. Nami naongea kitu ambacho nimefanya na si kusikia wala kusimuliwa. Hivyo mwanangu kazi kwako si kulaumu. Piga moyo konde ubadilike utabadili maisha yako.
 
It depends wamerudishwa Vipi .kama walikuwa hawana Ada ya shule? USA is the land of opportunity street smart is the way to go.ukitaka kitu chochote hapa unapata hakuna madeal.its about your choices
Natalia tushike mkono nasi tuje, unanihamasisha, na kweli USA nawapenda sana kwenye biashara hamna longolongo kama East, wanakupa mzigo kwanza unauza unawapa chao siku zinaenda sio hao wa East pesa kwanza ndo wakupe biashara
 

That is true.
Hii kujisomesha ni rahisi mno kuitamka na ni ngumu kui practice. Wee umeishi marekani unafahamu hili. Chukulia mtu ameingia marekani leo kutoka bongo na hana ada ya shule na ana mpango wa kubeba box ili aingie shule, pay check yake ya week ni dola ngapi na ada ni kiasi gani, na atafanya kazi kwa muda gani bila kutumia cent tano hadi ada itimie. Na unajua huku pia kuna bills za kulipa, na kama alikuja bila hela ujue mara nyingi ametoka kwenye familia ambayo haina pesa za kutosha na ujue huko bongo watu wanamtegemea pia.
Mtu kama huyu mpaka aje ku-settle inachukua muda mrefu, na katika huo muda anaweza akapata bahati mbaya na akarudishwa nyumbani akiwa hana kitu. Utamlaumu kivipi huyo mtu?
Halafu kibaya zaidi walewale uliokuwa unawatumia hela ndio wanakuwa wa kwanza kusema jamaa karudi bila kitu, wanasahau pengine wao pia walikuwa wana ku-set back.
 
Ni ujinga na upumbafu kuona utakaa marekani na kufanikiwa....wakome kuwa na mawazo ya kibaharia kama mtu flani hivi humu jf iliyekaa marekani miaka lukuki mwisho wa siku anakuja tz kutaka kuwa mjumbe wa nec....

mkuu umeua mno,!jamaa ni tikiti maji haswaaaa!
 

Assessment yako ni nzuri na inaukweli kidogo
 
Usimbeze nadhani anatoa ushauri kuhusu umuhiu wa kusoma. Vijana shikeni elimu. Anachosema mtoa mada ni sahihi kabisa. Angalia jjirani zako wenye maisha mazuri angalau kidogo ni wale waliosoma. Elimu ni ufunguo wa maisha.
 
Bongo tambalale bana maadamu akili mukichwa,nashukuru uamuzi wangu nilioufanya wa kurudi bongo fasta baada ya kuona mambo si mambo huko majuu,maisha yamekuwa mazuri zaidi bongo kuliko huko nilikokuwa na nimewaacha jamaa wako hoi kimaisha na hawataki kurudi bongo,utafikiri wana kesi za mauaji,kila kukichwa ni kuombana vijisenti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…