Baada ya kupata matatizo, mchumba wangu akaolewa na mfanyakazi mwenzangu

Wakuacha

JF-Expert Member
May 19, 2015
2,041
1,323
Habari wana JF,

Ni siku nyingine tulivu namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya Leo maana wengi walitamani lakini hawajafanikiwa kuiona na wengine wapo mahospitalini eeh Mungu wasaidie wapone.

Katika maisha wanawake si wa kuwaamini kwa asilimia 100 zote hapana kabisa. Mwaka 2009 niliajiriwa baada ya kuanza kazi mwaka huo 2009 nilijikita zaidi katika kujiendeleza kielimu nilijiunga na Chuo Kikuu huria na hatimaye mwaka 2012 nilihitimu Degree yangu.

Mwaka huo waliajiriwa wafanyakazi wengine walikuwepo ma binti kadhaa pamoja na wanaume kadhaa kama ilivyo wafanyakazi wanapoajiriwa kidogo mambo yao huwa yanakuwa hayajakaa sawa sawa. Nilitokea kumpenda binti mmoja kati ya wale wageni nikasema huyu ndiye na lazima atakuwa mke wangu.

Kiukweli nilimpenda na hata yeye pia alinipenda uhusiano wetu ulikuwa imara baadae mimi na yeye tukawa tunatembeleana kwa kuwa naye alikuwa amepanga nikawa naenda kwake nalala au yeye anakuja analala kwangu.

Mwaka 2013 mwezi wa 11 nilipatwa na matatizo kazini na kupelekea kufikishwa mahakamani kwa kosa la MAUAJI, wakati nikiwa gerezani nikisubiria vikao vya jaji kwa sababu mimi nipo pembezoni mwa Tanzania.

Nilikaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa ndio jaji alikuja na kuanza kusikiliza kesi yangu katika kipindi chote hicho huyo mchumba wangu alikuwa akija na kuanza kunifariji sana Mara nyingi alikuwa akija siku za Jumapili pale Gerezani aliniahidi atanivumilia.

Kwa kuwa mshahara ulikuwa ukiendelea kusoma nilimkabidhi kadi yangu ya bank na vitu vyangu vyote nilimkabidhi yeye, mwaka 2015 mwanzoni ndipo nilipatikana na HATIA YA KUUA BILA KUKUSUDIA na nikahukumiwa kwenda Jela miaka 5, alilia sana huyo mchumba wangu nilimsihi asilie maana hii yote ni mipango ya Mungu nilimuambia asijali mimi nitatoka tu maana HAKI YA MTU HUWA HAIPOTEI.

Wakati nipo Gerezani baada ya hukumu ile akaanza kubadilika nilikaa mwezi mzima bila kumuona nikaanza kusikia kwa watu kuwa mchumba wako yule Fred ambaye ni mdogo wako kikazi nasikia wanatoka niliumia sana kusikia vile niliamua kukata Rufaa na bahati nzuri niliachiwa huru mwaka Jana.

Niliwakuta tayari wamwashaoana na wanaishi kama mke na mume nilimfuata nikamuambia anipe vitu vyangu kwa aibu yule dogo alijificha chumbani, nilichukua vitu vyangu na kuondoka pale.

Tufanyeni kazi lakini watu sio wazuri pata matatizo ndo utajua nani ni mchumba/mke wa kweli.
 
Habari wana jf.

Ni siku nyingine tulivu namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya Leo maana wengi walitamani lakini hawajafanikiwa kuiona na wengine wapo mahospitalini eeh mungu wasaidie wapone.

Katika maisha wanawake si Wa kuwaamini kwa asilimia 100 zote hapana kabisa..Mwaka 2009 niliajiriwa baada ya kuanza kazi mwaka huo 2009 nilijikita zaidi katika kujiendeleza kielimu nilijiunga na Chuo kikuu huria na hatimaye mwaka 2012 nilihitimu Degree yangu..

Mwaka huo waliajiriwa wafanyakazi wengine ...walikuwepo ma binti kadhaa pamoja na wanaume kadhaa kama ilivyo wafanyakazi wanapoajiriwa kidogo mambo yao huwa yanakuwa hayajakaa sawa sawa..Nilitokea kumpenda binti mmoja kati ya wale wageni nikasema huyu ndiye na lazima atakuwa mke wangu...

Kiukweli nilimpenda na hata yeye pia alinipenda uhusiano wetu ulikuwa imara baadae Mimi na yeye tukawa tunatembeleana kwa kuwa naye alikuwa amepanga nikawa naenda kwake nalala au yeye anakuja analala kwangu.

Mwaka 2013 mwezi Wa 11 nilipatwa na matatizo kazini na kupelekea kufikishwa mahakamani kwa kosa la MAUAJI...wakati nikiwa gerezani nikisubilia vikao vya jaji kwa sababu Mimi nipo pembezoni mwa Tanzania.....nilikaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa ndio jaji alikuja na kuanza kusikiliza kesi yangu katika kipindi chote hicho.....Huyo mchumba wangu alikuwa akija na kuanza kunifariji sana Mara nyingi alikuwa akija siku za jumapili pale Gerezani aliniahidi atanivumilia...

Kwa kuwa mshahara ulikuwa ukiendelea kusoma nilimkabidhi kadi yangu ya bank na vitu vyangu vyote nilimkabidhi yeye ...mwaka 2015 mwanzoni ndipo nilipatikana na HATIA YA KUUA BILA kukusudia na nikahukumiwa kwenda Jela miaka 5...alilia sana huyo mchumba wangu nilimsihi asilie maana hii yote ni mipango ya mungu nilimuambia asijali Mimi nitatoka tu maana HAKI YA MTU HUWA HAIPOTEI.

Wakati nipo Gerezani baada ya hukumu ile akaanza kubadilika nilikaa mwezi mzima bila kumuona nikaanza kusikia kwa watu kuwa mchumba wako yule Fred ambaye ni mdogo wako kikazi nasikia wanatoka....
niliumia sana kusikia vile niliamua kukata Rufaa na Bahati nzuri niliachiwa huru mwaka Jana....niliwakuta teyari wamwashaoana...na wanaishi kama mke na Mme nilmfuata nikamuambia anipe vitu vyangu kwa aibu yule Dogo alijificha chumbani.......nilichukua vitu vyangu na kuondoka pale


Tufanyeni kazi lakini watu sio wazuri pata matatizo ndo utajua Nani ni Mchumba/mke Wa kweli....


View attachment 402317
Mkuu hii story yako kama ni kweli pole. Kama sio kweli mungu anakuona. By the way hiyo picha ya mrembo uko chini inahusiana na nini?
 
Huyo kwenye picha ndio mdada mwenyewe au? pole sana ila sijui ulitakaje lakini ukiwa kam mwanamme nilazima upambane na ukubaliane na matokeo,chakufanya ungemwambia baada ya hukumu kua wewe ndio ukondani na miaka mitano sio midogo,bora umuwache atafute maisha yake sasa ingekua mtihani kwake kama angekusubiri au angesonga mbele ingekua yeye,na kama walivyo baathi ya wanawake na wanaume pia wako,au angekua na uhakika gani baada ya kutoka ungebakia nae au ungepata mwengine?

Usimlaumu sana chamsingi umesha jua na utakua umejifunza,usimchukie kwani malipo ni hapa hapa Duniani..
 
ni kisu balaa. ili usingeweka picha yake hapa. Pole sana we fanya kazi kwa bidii ivi viumbe vipo tu. Ila kumvumilia mtu bila kufanya 5yrs yataka moyo so usimlaamu sana
Nilimpa kila kitu pesa na kadhalika....hiyo picha haiusiani na hii kitu
 
pole sana mkuu sasa hyo picha hapo ndio huyo dada? kama ni yeye au mfano wake acha tu aolewe aisee....

la msng anza upya na maisha yako usilaumu sana why ameolewa na mtu mwengine jarbu kuona tu katika mazingira ya kawaida unahis five years in jail huyu binti angekaa anakusubir tu wewe wakat hamkua na commitment yoyote zaid ya mahusiano ya kawaida?
 
pole sana mkuu sasa hyo picha hapo ndio huyo dada? kama ni yeye au mfano wake acha tu aolewe aisee....

la msng anza upya na maisha yako usilaumu sana why ameolewa na mtu mwengine jarbu kuona tu katika mazingira ya kawaida unahis five years in jail huyu binti angekaa anakusubir tu wewe wakat hamkua na commitment yoyote zaid ya mahusiano ya kawaida?
Nimekaa Gerezani kama miaka miwili tu....
 
ilikuwaje hiyo mpaka ukatuhumiwa kuua bila kukusudia?
Nadhan amesema hiyo kama sababu ya yeye kwenda jela,ila stori kuu ni usaliti kwenye mapenzi.
Any way ilishapangwa jamaa asifunge ndoa na huyo bintn sidhan kama kuna cha kulalamika,
 
ndio myaone.....hahahahha. wewe mwanamke ni wakugegeda tuu wala sio kujithaminisha ata siku moja.
 
  • Thanks
Reactions: dtj

Similar Discussions

Back
Top Bottom