Baada ya kumtongoza

Baada ya kumtongoza

Crystal field theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
951
Reaction score
412
Habari zenu wakuu,

Natumaini mu wazima katika Sunday hii, imenitokea kumpenda dada mmoja ambaye ni muuza mihogo na tambi katika chuo chetu hapa mjini. Katika harakati za kumpa namba nilimpa P6 yangu aandike namba..

Siku ya 4 nikamtongoza akasema OK. Baada ya figisu figisu za kutongozana akasema hana simu namsaidiaje? Wakati tunachat akasema narudisha simu sio yangu..

Msaada jamani hapo kuna mapenzi kweli?

Karibuni
 
kama hana simu mnunulie nyingine
 
Kama una hela si umnunulie simu?Si umemtongoza mwenyewe!Siku hizi mapenzi gharama ukiona huwezi., Tulia usome!
 
Ulivyoompa simu yako andike number yake mwenyewe, umejionesha kwake na yeye kakuona kwa hiyo anataka na yeye simu. Kama unauwezo hata usifikirie mara mbili mnunulie/mpe tu, lakini kama una pesa za mawazo tafuta ustaarabu sehemu nyingine kimya kimya kabla hujaaibika.
 
Pole sana ndugu,

Unaonekana ni mgeni sana kwenye maswala ya mapenzi.Kama kijana mzima mwenye akili timamu, maswala ya mapenzi huwezi kuyakwepa, ni jukumu lako kujitahidi kutafuta mwenzio ambaye yuko kifikra za mapenzi kama wewe na sio kuvamia vamia mtu yeyote. Kwa ufupi, huyo dada ni "GOLD DIGGER"

Mwisho, ningekuomba uzingatie masomo pia kwani bila kisomo, maisha yako yatakumbwa na misukosuko mingi...

Kila la kheri!!
 
Umenichekesha mkuu mweeeee..... sikia mapenzi yapo hapo ila tatizo mpenzi hana simu so fanya mpango huo umtafutie
 
Wewe dogo toa unafiki yaan umejisogeza ukamalize mtaji wake wa miogo? maana utaanza kula bure shenzi kasome kwanza.
 
Dah dongo hata kuandika haujui...!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Maliza Chuo kwanza. Sio kumaliza tu - upate pass bora na si bora umepass. Hayo mengine utakuja kuyakimbia mwenyewe mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom