Baada ya kumkamata mchina*(ubaguzi) wenye mabwawa ya samaki, wafugaji na wamwagiliaji, eti kina cha maji kimeongezeka!

Kwahio huyo waziri mpenda sifa na Magu hawatofautiani sana,kama Jinsi alivyo okota vichwa vya treni pale bandarini?
Ni pipa na mfuniko!!msanii tu, jana anaulizwa kuhusu Ponds za samaki, hizo 26, ambazo wawekezaji wana vibari, vya kutumia maji hayo, anakimbia kimbia tu!!zigo anaenda kutwishwa mtendaji wa kata eti alikuwa wapi, watu wanatumia maji ovyo!!sasa watu wana vibali toka bodi ya bonde husika wewe mtendaji unasauti ipi tena?!!
 
Nikisema kuna watu ni Wapuuzi naambiwa eti Mimi sio Mzalendo, asante sana mleta mada
 
Duu kumbe hata mabwawa ya kuhifadhi maji hakuna ?
Hao wataalamu bogus kabisa na mawaziri wote wa maji wamepita bila kuliona hilo

Sikulijua hili poleni sana
Tuanze na sisi wenyewe at individual level, Je huwa tunavuna kiasi gani cha maji msimu wa mvua kutoka kwenye maji yanayotiririka kwenye mapaa ya nyumba zetu? Kwa maoni yangu Nchi yetu haiwezi mudu Gharama za kutengeneza bwawa la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya watu milioni 5 wa jiji la Dar kutumia mwaka mzima
 
Maji ya Mtera huwezi kupeleka Dodoma kwasababu ndiyo hayo yakitoka hapo yanaenda kuzalisha umeme kwenye bwawa la kidatu. Ukipeleka Dodoma ina maana bwawa la kidatu life.
 
Hahaha walifanya maamuzi ya kidwanzi, walidhani wangelisha taifa kwa chakula walichohifadhi watu mia!! Tena kwenye vigunia kumi, ishirini!
 
Wewe at individual level huwa unavuna kiasi gani cha maji msimu wa mvua? Unajua gharama za kutengeneza bwawa la kuvuna maji ya mvua kwa ajili ya watu milioni 5 wa jiji la dar?
Kwahiyo serikali haina uwezo wa kujenga bwawa! Kwa taarifa yako serikali inao uwezo huo.
 
Kwahiyo serikali haina uwezo wa kujenga bwawa! Kwa taarifa yako serikali inao uwezo huo.
Mkuu, serikali yenyewe hapo ilipo ina madeni ambayo hata hatujui yataisha lini. Ukiachana na madeni bado kuna vipaumbele vingine vingi sana. Inawezekana lkn at the expense of other priorities au tuongeze tozo
 
Mkuu, serikali yenyewe hapo ilipo ina madeni ambayo hata hatujui yataisha lini. Ukiachana na madeni bado kuna vipaumbele vingine vingi sana. Inawezekana lkn at the expense of other priorities au tuongeze tozo
Tangu tumepata uhuru wangeweza kujenga endapo wangekuwa na akili hiyo, wao walibakia na walichoachiwa na mwingereza.
 

Kwa kweli hakuna tu
Maana kuhifadhi pipa la maji huko sio kuvuna na ndio wengi wanategemea pipa na madebe na ndoo tu

Kwa serikali Ina uwezo huo na zaidi ya hapo mkuu ila nani wa kusimamia na kutoa mwongozo?

Tatizo letu mambo hayaendi bila kufokewa na kutumbuliwa sijui kwa nini
 
Ukweli Ni kwamba sehemu nyingi Dar hakuna maji.
Jiongelesheni mtakavyo mkitegemea mileage za kisiasa lakini magonjwa ya mlipuko yatakapoanza ndio ukweli utakapo jitenga na blah blah za kufanya vikao vya kukurupuka usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…