Baada ya kumkamata mchina*(ubaguzi) wenye mabwawa ya samaki, wafugaji na wamwagiliaji, eti kina cha maji kimeongezeka!

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Mamlaka ya maji inajitapa kuwa baada ya kuwakamata waliokuwa wanachepusha maji imewasha mtambo wa Ubungo baada ya kina cha maji kuongezeka!

Sijui ni utaalamu gani huu au ni siasa. Kina cha maji kinawezaje kuongezeka wakati yanakoanzia maji hakuna ongezeko la maji!

Jibu tutalipata wiki ijayo mgao wa maji utakapo isha.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Mamlaka ya maji inajitapa kuwa baada ya kuwakamata waliokuwa wanachepusha maji imewasja mtambo wa Ubungo baada ya kina cha maji kuongezeka! Sijui ni utaalamu gani huu au ni siasa. Kina cha maji kinawezaje kuongezeka wakati yanakoanzia maji hakuna ongezeko la maji! Jibu tutalipata wiki ijayo mgao wa maji utakapo isha.

Eti kwa sababu ya mchina huyo na kina kwenye mabwawa ya kufua umeme kimeongezeka 😁😁:

IMG_20211121_091817_559.jpg

Hiiiiii bagosha!
 
Wakabambee58

Senior Member
Aug 14, 2020
114
250
Mamlaka ya maji inajitapa kuwa baada ya kuwakamata waliokuwa wanachepusha maji imewasja mtambo wa Ubungo baada ya kina cha maji kuongezeka! Sijui ni utaalamu gani huu au ni siasa. Kina cha maji kinawezaje kuongezeka wakati yanakoanzia maji hakuna ongezeko la maji! Jibu tutalipata wiki ijayo mgao wa maji utakapo isha.
Naomba unisaidie hapa, mtambo wa Ubungo unategemea maji, mafuta au gesi?
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Yule mchina walitakiwa wampakie na vumbi la mkongo wampelekee moto kabisa.
Mchina asiwe sababu, wao wametumia mchina ili kukuza hisia kuwa mgeni anaihujumu nchi! Uzembe wa serikali kutokuona umuhimu wa kujenga bwawa la kuhifadhi maji, wao hawakujua hasara kuachia maji yajiendee baharini! Haiingii akilini jini la Dar es Salaam kutokuwa na bwawa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi! Waziri Mkuu alikagua chanzo cha maji Dar lakini hakufikiria kujua kama kuna bwawa la kuhifadhi maji ila alichofikiria ni kuwatafuta wanaochepusha maji! Watazuia wote wanaochepusha maji lakini hawatayatumia maji yote watakayoyapata kwani yatapita kwenye mtambo na kuelekea baharini.
Tatizo la maji Dar limekuwa likiongelewa tangu miaka ya sabini, na viongozi wa wakati ule hawakufikiria kuhusu kujenga bwawa ila wao walifikiria kuchukua maji toka mto Rufiji, na wengine watakuja na mpango wa mto Ruvuma.
Tuwaangalie wakikimbizana na mito, wafugaji, wakulima na mchina*.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,885

Duu kumbe hata mabwawa ya kuhifadhi maji hakuna ?
Hao wataalamu bogus kabisa na mawaziri wote wa maji wamepita bila kuliona hilo

Sikulijua hili poleni sana
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Duu kumbe hata mabwawa ya kuhifadhi maji hakuna ?
Hao wataalamu bogus kabisa na mawaziri wote wa maji wamepita bila kuliona hilo

Sikulijua hili poleni sana
Ninakumbuka zamani mji wa Mbeya haukuwa na bwawa pamoja na maji kutiririka toka milimani, mji wa Iringa pia wanakinga maji kwenye mto Ruaha badala ya bwawa, Morogoro Mindu lilijengwa miaka ya tisini mwanzoni, nalo linanaharibiwa na wachimba dhahabu hivyo halijafikia lengo, Tabora Gombe lilijengwa na mwingereza kabla ya uhuru, Dodoma Mtera ingeweza kuipatia maji.
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
5,484
2,000
Mamlaka ya maji inajitapa kuwa baada ya kuwakamata waliokuwa wanachepusha maji imewasja mtambo wa Ubungo baada ya kina cha maji kuongezeka! Sijui ni utaalamu gani huu au ni siasa. Kina cha maji kinawezaje kuongezeka wakati yanakoanzia maji hakuna ongezeko la maji! Jibu tutalipata wiki ijayo mgao wa maji utakapo isha.
Kuishi Tanzania Ni kuona mengi.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
18,885
2,000
Ninakumbuka zamani mji wa Mbeya haukuwa na bwawa pamoja na maji kutiririka toka milimani, mji wa Iringa pia wanakinga maji kwenye mto badala ya bwawa, Morogoro Mindu lilijengwa miaka ya tisini mwanzoni, nalo linanaharibiwa na wachimba dhahabu hivyo halijafikia lengo, Tabora Gombe lilijengwa na mwingereza kabla ya uhuru, Dodoma Mtera ingeweza kuipatia maji.

Kweli mkuu hilo la Tabora nalijua na hata wilaya zake wana mabwawa ya Muingereza na yalikuwa maji yakitoka mto Igombe yanapita sehemu nyingi na ni mkondo mrefu ila yalikuwa yanafungwa kwa ukuta mkubwa ambapo kunakuwa na matundu
Yakifika juu yanamwagika tena kupitia hayo matundu makubwa

Kwa hiyo walimuona mzungu zuzu kama wao leo ama

Wameshindwaje miaka yote hiyo kuiga hivyo ?
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Kuishi Tanzania Ni kuona mengi.
Mji wa Moshi theruji inayeyuka na kutiririkia katikati ya mji, hakuna bwawa, kuna shida ya maji! Kenya wametengeneza chanzo cha nishati ya umeme kutokana na joto la aridhini! Sisi tunajenga bwawa huku Makambako, Same na Singida upepo ukitupepea.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
11,292
2,000
Inanikumbusha wakati wa Nyerere kulikuwa na uhaba wa chakula, msako ulifanyika majumbani kutafuta wanaoficha chakula, wakapatika wenye ndoo za mchele na unga tukawaita wahujumu uchumi, nafaka hizo zikapelekwa kwenye maduka ya bidhaa muhimu watu na mawe wakajipanga foleni kununua, waliofanikiwa kuuziwa watu wachache tu zikaisha, tatizo likabaki palepale mpaka mmarekani akatuletea yanga na mchina akaleta kitumbo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom