Baada ya kumaliza ndugu wanaompinga, alijimaliza mwenyewe

Baada ya kumaliza ndugu wanaompinga, alijimaliza mwenyewe

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,333
Reaction score
1,356
Alikuwa adui kweli wa ndugu wanaompinga (yaani wapinzani) alifanya kila namna kuwaua alivunja hata utamaduni wa kindugu wa kukutana Kwa tangazo haramu la kuzuia ndugu kukutana hadharani na hata chumbani Hakupenda pia aliwaua, kuwateka, kuwafunga, kuwajeruhi na kuwafilisi wanandugu, majirani na marafiki zao hakuacha kitu.

Aliwachukia wazungu (mabeberu) saaana lkn jeuri yake ya kujenga elephant projects ilitoka Kwa mabeberu, alikopa kimya kimya Kwa mabeberu huku hataki walipaji wajue.Mwenge wa uhuru? Hapana pesa yake ikajenge miundombinu.

Baada ya hayo aliwageukia wachama wake na kuwabatiza Kwa moto. Alikuwa mtakatifu, viongizi wa dini na waumini wao walifundishwa ucha Mungu kweli kweli.

Haki za binadamu zilikuwa ndio yeye, uhuru wa vyombo vya habari NGO's na kukoselewa ilikuwa jinai enzi zake. Haikupita sekunde BILA kumwona KWENYE tv. Yeye ndiye msomi, mwenye akili, uwezo wa kuongoza, mtetezi wa wanyonge, msema kweli, mpenzi wa Mungu na kiongozi wa malaika. Aliwahi kusema TUTAMKUMBUKA! yes! Kweli TUNAMKUMBUKA.

Waliokubaliana na mfumo wa vyama vingi hawakuwa wajinga, waliotutengenezea Katiba ya sasa hawakuwa wajinga, waanzilishi wa mwenge wa uhuru hawakuwa wajinga. Korana ilitikisa ulimwengu lkn kwake ilikuwa mafua. Na mafua hayo yaliwateketeza wasio na hatia wengi!

Mwishoni mwa janga la korona ghafla kukawa na sitofamu mara jembe lipo ofisini Lina kwangua kokoto. Mara kwene tv show Sasa anaonekana mama mwenye nyumba.

Duu! Binadamu tunajimaliza wenyewe. Kunywa pombe sana ni hatari Kwa afya Yako, kuvuta sigara sana ni hatari Kwa afya Yako, kuwa mzinifu ni hatari Kwa afya Yako, kudharau misingi ya taifa lako ni hatari Kwa uhai WAKO, kuwa MLEVI WA MADARAKA SANA ni hatari Kwa uhai WAKO. Utajimaliza mwenyewe, alijimaliza mwenyewe.

Roho ya uzalendo huo inaishi bado katikati mwetu BILA kurekebisha mambo IPO siku tutajiona wapuuzi sana Kwa pamoja kama Familia(Taifa).
 
USHAMBA TU.

Mimi nashaurii tuu, hili taifa lina mambo meeengi sana ya kuongelea apart from kulaumu mtu ambaye hawasikii wala kuona malalamiko yenu juu yake.

Kama taifa tunahitaji sera mpya na mawazo mapya ya kuinua uchumi wa raia na sio ngonjera za kutusimulia mabaya ama mazuri ya huyo bwana.

Kumsimanga huyo bwana, ni wazi kwamba aliwazid nguvu na akili ndiomaana kelele zimekuwa nying mpka kifo chake hiyo inaprove watu bado hawaamini kuwa jamaa aliwashinda kwa kila kitu.

Njoeni uraian maji ya shida, umeme wa mgao, bidhaa bei kubwa, pembejeo za kilimo bei ghali, wakulima wa korosho bei mbovu, wanafunzi shule hazina vitendea kazi, vijana mitaan hakuna ajira wala mikopo saidizi, zaidi zaid kuna ongezeko la rushwa, wizi wa kodi, lundo la wawekezaji uchwara na unyang'anyi wa ardhi za wazawa,

Hayo ndiyo ya kuyaongelea yasolvike sio hizo takataka na habari zenu za kizushi kuhusu huyo marehemu wenu asiyewasikia.

Raia hawali hizo stori za kusadikika wanahitaji huduma nzurii
 
USHAMBA TU.

Mimi nashaurii tuu, hili taifa lina mambo meeengi sana ya kuongelea apart from kulaumu mtu ambaye hawasikii wala kuona malalamiko yenu juu yake...
Huwezi kumaliza tatizo kama hujui chanzo Cha tatizo, matatizo ya Tanzania ni katiba mbovu inayozaa viongozi wa hovyo kama huyu tunae mtokea mifano.

Huyu ndio ametuonyesha ubovu wa katiba hii Kwa kiwango Cha kutosha,tutamtolea mfano mpaka tutakapopata katiba MPYA, hayo maji, huduma mbalimbali, miundombinu n.k chini ya katiba hii havitopatikana kamwe
 
Huku ndio kusadikika!!??
JamiiForums1747635565.jpeg

USHAMBA TU.

Mimi nashaurii tuu, hili taifa lina mambo meeengi sana ya kuongelea apart from kulaumu mtu ambaye hawasikii wala kuona malalamiko yenu juu yake...
 
Alikuwa adui kweli wa ndugu wanaompinga (yaani wapinzani) alifanya kila namna kuwaua alivunja hata utamaduni wa kindugu wa kukutana Kwa tangazo haramu ...
Mkuu Poa 2 , kuwa poa tu kama jina lako, pamoja na yote hayo, he was a human being hivyo ni kiumbe dhaifu na ni kweli kuna makosa alitenda, kuna dhambi alifanya ila kabla hajatwaliwa roho yake, alitubu, akasalishwa sala ya toba, na Baba Askofu fulani, akapakwa upako mtakatifu na Muadhama wa dhehebu lake, na kama haitoshi Sheikh Mkuu nae akampiga dua!, saa hizi yuko na Baba yake kule nyumbani kwa Baba Yake, haya yatoshe sasa tumwache apumzike!. Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 
Aliwanyoosha, hamtamsahau kamwe.
Ni kweli hatasahaulika kamwe! Shetani lini kasahaulika kwa mambo yake?

Nenda Germany, why Hitler anatajwa leo mtu aliyekuwepo miaka 80 iliyopita?

Mobutu, Nguema nk wamesahaulika? Hapana, na ni kwa matendo yao. Na huyu naye anatajwa sana ili asijetokea mtu mwingine tukampa nafasi akawa kama yeye!

Kunyamaza ni kukubaliana na aliyokuwa anafanya yaliyokuwa ya kishenzi. Na ashukuru corona imemuondoa kistaarabu, watu kama yeye karibu wote huishia namna zile za Samwel Doe, Saddam nk.

Suala la upungufu na shida hizi za sasa ni wazi lilikuwa lazima lije, baba gani anaridhisha familia yake kwa kukopa fedha kwa siri?

Anakopa sana kwenye mabenki huku vitu viletavyo pesa kama korosho anaviua hiyo nayo akili?

Watu (hasa wafuasi wa sukuma gang) wanalaumu upinzani eti ndio wanamsema huyo mwenda zake, lakini ukweli wao wanakazia tuu hasa kuhusu ukatili binafsi aliokuwa anafanya, lakini wana CCM walio madarakani ndio hasa wanamlaumu kwa kuharibu uchumi na mipango mizito isiyokuwa na plan aliyo ianzisha jinsi inavyo wapa shida.

Haya matozo ni uzao wa jiwe kwa sababu vyanzo aliviua na madeni yameiva wangefanyaje?
Wanaopinga asisemwe ndio wanachochea ASEMWE SANA.
 
Mkuu Poa 2 , kuwa poa tuu kama jina lako, pamoja na yote hayo, he was a human being hivyo ni kiumbe dhaifu na ni kweli kuna makosa alitenda...
Vipi kuhusu wanaofuatia? Tunayo nafasi ya kumsema ili wanaofuata wasiige mfano mchafu wa marehemu eti wakijua nikitaka kufa ataitwa Pengo na Sheikh Zuberi nami nitaenda peponi kuwa mkuu wa malaika!

Huo ni ubinafsi mkubwa, tutamsema ili liwe fundisho kwa viongozi wanaofuatia.

Hata waandishi wa vitabu tunawaomba waandike sana vitabu vya kumuelezea uzuri wake na mabaya yake kwa faida ya vizazi vijavyo Tanzania na duniani pote.
 
Ukapimwe afya ya akili

Miaka miwili sasa , bado unamlaumu marehemu
Kifo kitakukuta bado unalaumu

Mi nazani unge mlaumu Mama yako kukubali kuolewa na mtanzania maskini

Tanzania hakuna Upinzani ni makundi ya Wendawazimu waliojikusanya pamoja wasioelewa wanataka nini, na kamwe hawatokuja kuongoza nchi hii
 
Back
Top Bottom