enery
JF-Expert Member
- Aug 21, 2015
- 368
- 437
Katika hotuba yake kwa Bunge la Urusi mnamo tarehe 18 Aprili 2014, ambapo Rais wa Urusi Putin alithibitisha kuingizwa kwa Crimea katika nchi ya Urusi na kuwa sehemu ya Urusi, alisisitiza udhalilishaji wa Russia uliotoka kwa sababu ya ahadi nyingi zilizoharibika na zinazo endelea kuhaibiwa na Magharibi, ikiwa ni pamoja na ahadi ya kudai kutokukua NATO zaidi ya mipaka ya Ujerumani.
Upanuzi wa NATO kwa Georgia na Ukraine unahatarisha usalama wa nci ya Urusi, Rais Vladimir Putin alisema katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Fox News "Chris Wallace", muda mfupi baada ya mkutano wake na Rais wa U.S.A Donald Trump huko Helsinki mnamo Julai 16, 2018.
Alipoulizwa nini msimamo wa Kremlin ikiwa Georgia na Ukraine watakubali kuingia katika shirikisho la NATO, Putin alisema kusogea kwa miundombinu ya kijeshi ya NATO karibu na mipaka ya Urusi inaweka "tishio la moja kwa moja" kwa usalama wake na kwamba itaangalia mchakato wa kufanya na hakika utakuwa ni msumali na mwiba kwa upande wa shirikisho hilo akisisiiza kuwa utakuwa "mbaya sana."
Maneno haya ya Vladimir Putin yanajitokeza chini ya wiki baada ya Azimio la Mkutano wa Mkutano wa Brussels, ambayo ilielezea uamuzi uliofanywa katika Mkutano wa Bucharest wa 2008 "kwamba Georgia itakuwa mwanachama wa Muungano wa NATO.
Ukweli napenda sana kuwa na washirika wazuri kama Cuba maishani mambo yakienda kombo ukizungumza nae anakuelewa. Baada ya Missile crisis warusi waliondoka Cuba, na sasa mgogoro mkubwa unaendelea duniani wameamua kurudi tena Cuba na Wacuba wamewapokea na mikono miwili na jamaa wanafunga tena mitambo yao kuweza kum monitor Mmarekani pamoja.
Ukweli Putin ni kiongozi mwenye maono ya mabli na kutafakari kwa kina, endapo zisingekuwa busara za Putin kwa sasa dunia ingekuwa si sehemu salama hata kidogo, ila mara nyingi hutulia na kufanya maamuzi kwa mustakabali wa dunia. Mathalani wamarekani na washirika wake wawili wasijitambua wale Uingereza na Ufaransa walivyopiga Syria mwezi april angeamua kujibu basi dunia ingekuwa pabaya mpaka sasa