Baada ya kikombe cha babu, sasa dhahabu yagundulika Samunge

Baada ya kikombe cha babu, sasa dhahabu yagundulika Samunge

Wanahabari potezeeni hii issue.Tunayo mambo mengi hapa nchini kwa sasa hatujayapatia majibu.mf kifo cha bosi wa EWURA
 
Naenda huko ole wao Mwananchi mnidanganye. Wahariri nitawageuza nyani warudishe hela kwa njia ya utalii
 
Kweli nimeamini watanzania mazezeta yaani m'metolewakwenye mada harisi tena ya msingi ktk mustakabari mzima wataifa.juu yakatiba na kupelekwa kusikojulikana ili watu wachaaache wafanye vitu vyao.mkishastuka mambo yamekwisha. Na kubaki mkilalamika tu. Bila kujuwa nn cha kufanya acheni hizo rudini kwenye utetezi wataifa letu tupate katiba yenyemanufaa . Mulishadanganywa nilifikili kuwa mtaelimika kumbe bado ni watoto wenyekudanganywa na pipi ya kijiti !!!?
 
Arusha. Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika katika eneo hilo.

Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.

Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.

“Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka, hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba,” alisema Sandea.

Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.

“Kuna wengine wanapata hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi,” alisema.

Ulinzi waimarishwa

Diwani huyo alisema ulinzi umeanza kuimarishwa katika eneo hilo akisema hali ikiachwa kama ilivyo, kunaweza kutokea vurugu kubwa na hata mauaji.

“Sisi kama viongozi, tumeweka utaratibu mzuri wa kuchimba madini kiusalama na hata wale ambao wameanza kuuza mashamba yao, tunawawekea utaratibu mzuri,” alisema.

Maofisa madini kutua Samunge

Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Alex Magayane alisema jana kwamba baada ya kupokea taarifa za kugundulika kwa dhahabu katika eneo la Samunge, maofisa wake wanajiandaa kwenda kijijini hapo.

Alisema taarifa za kitaalamu kuhusu akiba ya madini hayo iliyopo Samunge itatolewa baada ya maofisa hao kufika katika eneo hilo na kufanya utafiti.

Ahadi ya Babu

Kugundulika dhahabu katika eneo hilo kunahusishwa na ahadi ya Mchungaji Mwasapila kuwa mamilioni ya watu watafika tena Samunge baada ya kupungua ikilinganishwa na miezi ya mwanzo baada ya kuanza kutoa tiba ya kikombe cha dawa iliyodaiwa kutibu magonjwa sugu.

Tiba yake hiyo ambayo ilizua utata kitaalamu na ikielezwa kuwa waliotibiwa waliugua tena na wengine kupoteza maisha, aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema watu kutoka mataifa yote watakwenda tena Samunge siyo kupata kikombe pekee, bali huduma nyingine.

Licha ya wengi kuitilia shaka kauli yake hiyo, aliendelea kuisisitiza na akikata miti na kujenga kituo kikubwa cha kutolea huduma ya kikombe.

Source: Mwananchi

bado almasi
 
nasema hv! bado naitaka tanganyika yangu.kuhusu kwa babu samunge ctaki kujua.

Nakuunga kichwa sio mkono tena, ili uwe na msimamo huo huo, hili la dhahabu limetengenezwa kupoteza hoja Tanganganyika, kama ilivyokuwa sh. bln 95. ya Dowans na kikombe cha babu acha weee.
 
kwel watanzania akil milege! Hii n mirusi ming na itawapoteza kwenye misimamo!
 
huko loliondo kazi moja tu kuondoa watanzania kwenye ajenda ya Tanganyika kama ya billion 95 shs ya Dowans miaka ileeeee na mjadala ukaishia pale!
 
Back
Top Bottom