Baada ya kesi kuwa ngumu, kampuni za Patrice Motsepe zimeanza kuomba "kinga" kutoka Afrika Kusini dhidi ya mahakama za Tanzania

Baada ya kesi kuwa ngumu, kampuni za Patrice Motsepe zimeanza kuomba "kinga" kutoka Afrika Kusini dhidi ya mahakama za Tanzania

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Bilionea Patrice Motsepe na baadhi ya kampuni zake wanatuhumiwa kujaribu kutumia mahakama za Afrika Kusini kukwepa uamuzi wa kesi unaotarajiwa kutolewa nchini Tanzania kuhusu mgogoro wa uchimbaji madini.

Mgogoro huo unahusisha kampuni ya Tanzania ya Pula Graphite.

Kampuni ya Pula imedai kuwa, mwaka 2019, walisaini makubaliano ya kutunziana na kulinda siri za biashara na kampuni za Motsepe

Hata hivyo, Pula imedai makubaliano hayo yalikiukwa na kwamba kampuni za Motsepe zilitumia siri hizo za kibiashara kuwekeza kwenye mradi wa uchimbaji wa graphite katika eneo la Ruangwa, Tanzania.


Baada ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa nchini Tanzania ilipofika Agosti 2025, kampuni ya Motsepe inayoitwa African Rainbow Capital (ARC), ilienda Mahakama Kuu ya Johannesburg peke yake bila kuijulisha kampuni ya Pula

Soma zaidi > Rais wa CAF, Patrice Motsepe ashtakiwa Dar es Salaam, Kesi ya Tsh. bilioni 525.8 kuunguruma leo Novemba 4, 2024

ARC iliomba ruhusa (kwenye mahakama hiyo mahakama ya Afrika Kusini) ya kupeleka nyaraka za kesi kwa utaratibu maalum huku ikisema kuwa haikuweza kupata nafasi ya kuzungumza na kampuni ya Pula kabla ya kufungua kesi.
Baadaye, mwezi Desemba, ARC iliomba kesi hiyo ianze kusikilizwa kama kesi ya kibiashara na isikilizwe kwa haraka.


Pula imedai kuwa kitendo cha ARC kufungua kesi Afrika Kusini kunalenga kuchelewesha kesi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa mahakama ya Tanzania inatarajiwa kupangia kesi hiyo tarehe ya kusikilizwa ndani ya miezi miwili ijayo.

Ikumbukwe kuwa kampuni yaa Pula ilifungua kesi hiyo mwaka 2023 na pia ikamtaja Patrice Motsepe, African Rainbow Minerals (ARM), na ARCH Sustainable Resources kama wahusika wengine katika mgogoro huo.

Aidha ikumbukwe kuwa Patrice Motsepe ambaye pia ni Rais wa CAF, mwezi Novemba 2025 alimpatia tuzo Rais Samia kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya soka nchini

motsepe.png


===========================================

Billionaire Patrice Motsepe and several of his companies have been accused of seeking protection from SA courts from an imminent ruling in Tanzania in a mining dispute, in which he and several Motsepe-linked companies stand accused of breaching a confidentiality agreement signed in 2019 with Pula Graphite in Tanzania.

In August 2025, one the respondent companies, African Rainbow Capital (ARC), approached the Joburg High Court on an ex parte basis (where only one side argues) for an order allowing it serve papers by way of edictal citation, where an opponent’s whereabouts are unknown.

In December, ARC wrote to Justice Sutherland of the Joburg High Court, requesting that its application be designated a commercial court matter and set down for an expedited hearing.

Pula says these are transparent delaying tactics by Motsepe and his companies, as the Tanzanian court is expected to set down a trial date within the next two months. The other parties named in the case by Pula are Motsepe, African Rainbow Minerals (ARM), and ARCH Sustainable Resources.

The case was brought by Pula in 2023 over an alleged breach by of a non-disclosure agreement (NDA) that gave Motsepe’s companies access to Pula’s confidential information, which was then used to invest in a rival graphite project in the Ruangwa region of Tanzania.

Source: Money Web
 
Duh huko southern Tanzania kuna utajiri wa kufa mtu lakini umaskini ndio jina lao,CCM hawawezi kazi waachie wengine, hakuna sababu ya kuwa maskini wakati nchi ina utajiri mkubwa kama huu
 
Back
Top Bottom