Ni kweli mkuu hasa hapo kwenye REDMie nadhani haka katabia ka kuzuia-zuia ndio shida. Mara kuzuia watu wasioane kwa sababu hawana vyeti vya kuzaliwa, mara kuzuia mtu fulani asichaguliwe kwenye cheo fulani kwenye chama chake, mara kuzuia wasanii wasiimbe hisia zao, mara kuzuia mitandao.....n.k. Kama nia ilikuwa ni magazeti yanunuliwe agizo lingekuwa habari ziwe zinasomwa nusu ili watu wawe na shauku ya kununua magazeti wamalizie. Lakini ukizuia kabisa, hata habari ambazo serikali yenyewe inataka wananchi ambao hawana uwezo wa kununua magazeti wazisikie hazitawafikia hao wananchi. Kwa hivyo hiyo ban ya magazeti ni 'counter productive. Badala ya kuwahabarisha watu mambo ya nchi yetu, inawafanya watu wengi wasikilize mambo mengi ya uzushi mitaani maana ukweli hawaupati tena.
Hapo umenena. nimesahau kukupa like.Kama wangejua kwamba vile vipindi vya kusoma magazeti vilisaidia kutangaza biashara za wenye magazeti wala wasingelikataza kuyasoma
Poa usijaliHapo umenena. nimesahau kukupa like.
Naitafuta hiyo app sasa hv wakitaka waifungie!!!Kuna app ya m-Paper. Nasoma magazeti kuanzia saa 6 usiku linapotoka tu. Na Ukilipenda unalinunua kwa nusu bei. Mauzo yaongeze wapi?
Ile ilikua kiki tu mkuu.
Unaipataje hiyo?Kuna app ya m-Paper. Nasoma magazeti kuanzia saa 6 usiku linapotoka tu. Na Ukilipenda unalinunua kwa nusu bei. Mauzo yaongeze wapi?
Ile ilikua kiki tu mkuu.
Ingia google playstore ipoUnaipataje hiyo?
Ni kweli mkuu kitu unakisoma mtandaoni leo kinatoka kwenye gazeti keshoWatu wana-approach tatizo kutokea angle mbovu.
Wao kuona mauzo ya magazeti yameshuka, wamefikiri sababu ni magazeti kusomwa redioni na kwenye TV.
Siku hizi ni rahisi kupata habari kupitia mitandao ya kijamii kama vile JF kwa gharama kidogo. Hata hayo magazeti yanachukua habari kutoka kwenye hii mitandao ya kijamii. Ndio maana sasa hivi ukienda kwenye vibanda vya magazeti huwezi kukutana na habari mpya ambayo hujaisikia......Kwa mwendo huu ni nani atanunua gazeti?