Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Baada ya Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga kushikiliwa Uwanja wa Ndege Dar majira ya saa 9 alfajiri alipowasili nchini kufuatilia kesi ya Tundu Lissu, Jaji Mkuu mwingine mstaafu wa nchi hiyo David Maraga, amefanikiwa kutinga Kisutu.
Pia soma Pre GE2025 - DSM - Kesi ya Lissu: Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga ashikiliwa uwanja wa Nyerere. Polisi waonekana Kisutu
Pia soma Pre GE2025 - DSM - Kesi ya Lissu: Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya Willy Mutunga ashikiliwa uwanja wa Nyerere. Polisi waonekana Kisutu
Hawa watu sijui wanawaza nini. Wameamua kumpa Tundu Lissu umaarufu over night!!! Sasa kesi hii inafahamika nje ya mipaka yetu. Sasa Lissu anazidi kujulikana zaidi na no reforms no election inavuka mipaka ya taifa letu.
Kilikuwa na sababu ya yote haya? Kilikuwa na sababu gani ya kumkamata na kumpaisha Lissu kwa kiwango hiki? Kuna sababu Gani ya kuendelea kumshukilia?
Ni kweli kumuachia kwa kuifiluta kesi hii itawachora mno waliomkamata Lakini kuendelea kumshukilia (ambako lazima TU watamuachilia baadaye) ni kuendelea kuharibi zaidi kitaifa na kimataifa. Lissu aachiliwe TU aendelee na siasa sake na reforms zifanyike, uchaguzi uwe huru na aliyepangiwa na Mungu kushinda ashinde kwa haki.
Kama Lissu alipangiwa kuwa rais wa nchi hii hakuna wa kuweza kuzuia hilo. Kama hakupangiwa hawezi Kuja kuwa Rais wetu. Tuache haya tunayofanya sasa kwa sababu yanaharibu zaidi kuliko kujenga
1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.
Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?
Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.
HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.
Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners!