bothlegs
Senior Member
- Apr 14, 2009
- 123
- 49
Muarabu mmoja anaeitwa FARAJA alikuwa mbabe sana katika mtaa aliokuwa akiishi.Watu wote pale mtaani walikuwa wanamuogopa.Yaani hakawii kutoa kichapo kwa yeyote yule atakaye gombana naye.Siku moja katika kugombana kwake akakumbana na Muhindi.Yule muhindi anaitwa DHIKI, alikuwa anamjua sana huyu Muarabu kwa ukorofi wake.Zikachapwa kavu kavu pale.Mwisho wa siku Muhindi akaibuka kidedea dhidi ya yule Muarabu.Kwa majisifu na magigambo yule kanji bhai akamwambia Mwarabu "Kama wewe FARAJA IKO MIMI DHIKI".Kwani swahili nasema BAADA YA DHIKI FARAJA.Akaendelea kujigamba sasa mimi nakuwa babe na wewe nafuatia.